Takriban watu 78 wamefariki dunia, baada ya Boti kupinduka katika Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapo jana.
Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini, Jean Jacques Purisi, amethibitisha taarifa hizo, na kuongeza kuwa watu 278 walikuwa wamepanda boti hiyo, kabla ya kupinduka.
"Itachukua angalau siku tatu kupata namba kamili, kwa sababu sio miili yote imepatikana," Purisi aliiambia Reuters.
Hata hivyo Gavana wa jimbo jirani la Kivu Kaskazini alisema takriban watu 58 wameokolewa.
Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED