Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika matumzi ya nishati safi, Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania (SHISAMA) limeamua kusaidia kutoa elimu kwa jamii kupitia majukwaa yao.
Ombi hilo limewasilishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu Shirikisho hilo Aloyce Makonde wakati akisoma risala yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa Pwani Abubakari Kunenge na kusisitiza sanaa ni kazi na ni biashara, na kwamba kundi hilo halipaswi kutengwa na serikali.
"Shirikisho linaomba Mkoa wa Pwani, utoe fursa kwa wasanii wa sanaa za maonesho Tanzania kupatiwa fursa za kutoa elimu ya masuala mbali mbali ya kijamii kupitia Sanaa" alisema
Aidha amesema Shirikisho linaomba ardhi kwa ajili ya kujenga Kituo cha Sanaa ili liweze kusaidia kukuza vipaji kwa wingi.
Akijibu hoja hizo, Ndemanga ameahidi kufukisha maombi hayo kwa Mkuu wa Mkoa, akisisitiza yapo ndani ya uwezo wake.
Kuhusu wasanii hao kuwezeshwa amesema kwakuwa zipo program za mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake na vijana itatoa kipaumbele kwa Wasanii.
Kuhusu Ombi la ardhi ya kujengea kituo hilo nalo amesema Serikali yake iko tayari kutoa ardhi ili SHISAMA iweze kutimiza malengo yake.
Aidha katika Mkutano huo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao pia ni waaandaaji wa mkutano huo Lilitoa elimu ya matumizi nishati Safi na salama ya kupikia na kuhamasisha watu kupanda miti.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED