Mwanamke apeleka maiti benki ili kupata saini ya mkopo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:16 PM Apr 18 2024
Mwanamke apeleka maiti benki ili apate mkopo.
PICHA: MAKTABA
Mwanamke apeleka maiti benki ili apate mkopo.

MWANAMKE mmoja nchini Brazili amezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii baada ya kupeleka maiti ya mzee katika benki, ili kupata saini ya mkopo.

Katika video iliyosambazwa mitandaoni mwanamke huyo alionekana akisukuma maiti ya mzee iliyekuwa imevishwa nguo nadhifu na kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu hadi kwenye eneo la wateja kuhudumiwa na kujaribu kumfanya atie saini karatasi iliyokuwa mbele yake.

Alimpa kalamu na kujaribu kumuita asaini karatasi hiyo lakini hakuweza kufanya hivyo.

Wafanyikazi wa benki walitilia shaka kichwa cha mwanamume huyo kikirudi nyuma wakati mwanamke huyo alipoacha kukishikilia na wakawapigia simu polisi, ambao walimkamata papo hapo kwa tuhuma za ulaghai. Maiti ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa mujibu wa Wakili wake alidai kuwa mwanamume huyo alifariki katika benki hiyo lakini uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa alikufa mapema, akiwa amelala chini.