Oryx yaendelea kuwawezesha watanzania kutumia nishati safi

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 07:24 PM Apr 30 2024
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Ges Tanzania Benoit Araman (kushoto), akimkabidhi jiko la gesi, mmoja wa waandishi wa habari, leo mkoani Dar es Salaam.
Picha Maulid Mmbaga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Ges Tanzania Benoit Araman (kushoto), akimkabidhi jiko la gesi, mmoja wa waandishi wa habari, leo mkoani Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Oryx Ges kwa kushirikiana na benki ya NMB inaendesha program ya kibubu iliyoanzishwa mahususi kwaajili ya kumuwezesha mtanzania kuwekeza fedha kidogo kidogo zitakazo muwezesha kupata mtungi wa Ges kwaajili ya kupikia.

Hayo yamebainishwa leo mkoni Dar es Salaam na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Peter Ndomba, wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi ya Ges na majiko kwa wahariri na waandishi wa habari, ikiwa ni muendelezo wa program ya Oryx ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema mwaka 2021 walianza jitihada za kuhakikisha kila kijiji nchini kinakuwa na walau msambazaji mmoja wa Ges, na kwamba kwa sasa wanaendeleza kampeni hiyo nyumba kwa nyumba, akibainisha kuwa nchini kuna takribani nyumba milioni 14 na kati ya hizo ni miliomi mbili tu zinazotimia nishati safi ya kupikia.

“Lengo letu ni kwamba angalau zifike nyumba milioni nane mpata tisa ambazo zinatumia nishati safi, na sasahivi tumeamua kwenda zile sehemu ambazo kuni zinatumika zaidi na kuhamasisha watu waachane na matumizi ya nishati chafu watumie Ges kupikia,” amesema Ndomba.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Ges Tanzania Benoit Araman, amesema hayo yote yanafanyika kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuiwezesha jamii ya watanzania kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanaathari kiafya na kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Kwa kutambua umuhimu wa nishati safi tumeamua kuibeba kampeni hii kwa ukubwa wake, Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza zamira yake ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, Oryx Ges tumedhamiria kwa vitendo kufanikisha ndoto ya rais,” amesema Araman.