WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemteua Christine Mwakatobe kuwa mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha, (AUWSA) kuanzia Mei 13 mwaka huu.
Mwakatobe kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano Arusha AICC.
Sehemu ya barua ya uteuzi inaeleza kuwa Waziri Aweso amemteua Mwakatobe, kwenye bodi hiyo nafasi ya mwakilishi wa watumiaji wakubwa wa maji jijini Arusha.
“Ni matarajio yangu kuwa utaupokea uteuzi na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha, iendelee kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu,” amesema Waziri Aweso
Katika barua hiyo Aweso amenukuliwa na kusisitiza kuwa Mwakatobe atatekeleza majukumu yake, kwa kuzingatia miogozo na maelekezo ya Wizara, Msajili wa Hazina na Serikali.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa AICC, Machi mwaka huu Mwakatobe ambaye kitaaluma ni mchumi na mtaalamu wa masoko, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro
KADCO.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED