Benki ya KCB yadhamini mbio za usonji ‘Run4Autism’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:36 PM Apr 30 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mbio za hisani za ‘Run4Autism’.
Picha: Benki ya KCB
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mbio za hisani za ‘Run4Autism’.

Katika kuunga mkono makundi mbalimbali na kurudisha kwa jamii, Benki ya KCB imedhamini na kushiriki mbio fupi za hisani za 'Run4Autism' Tanzania zenye lengo la kuongeza uelewa juu ya tatizo la usonji nchini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kama mgeni rasmi, alitoa pongezi za kwa Benki ya KCB Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono makundi jitihada mbalimbali kupitia uwekezaji kwa jamii.

Mkuu wa Idara ya Masoko, Uhusiano na Mawasiliano, Christina Manyenye akimuwakilisha Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Benki Tanzania, alisisitiza kuwa mbali na mafunzo ya ujuzi na ufundi ya 2jiajiri, KCB Benki Tanzania itaendelea kutekeleza azma yake ya kuigusa jamii na makundi mbalimbali kwa namna tofauti.

1
“KCB Benki tunaungana na Lukiza Foundation katika kuleta elimu ili wazazi wengi wajitokeze na kuwasaidia Watoto wenye tatizo la usonji nchini, tunaamini kupitia mbio hizi tunachangia katika kuleta mabadiliko Chanya kwa manufaa ya jamii yetu, alisema.

Kupitia mbio hizi, benki imeonesha dhamira yake ya kuunga mkono jitihada za kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa usonji na kuendeleza michezo nchini.

Mbali na hilo, benki ya KCB inashiriki katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwamo kusaidia vijana kielimu na kiujuzi kupitia programu ya 2jiajiri ambayo imekuwa chachu katika kupunguza tatizo la ajira.