Meta kizimbani athari Instagram kwa watoto

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:30 PM Feb 19 2026
news
Picha Mtandao
Meta kizimbani athari Instagram kwa watoto

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya teknolojia ya Meta, zamani facebook, Mark Zuckerberg, amepandishwa Mahakamani jijini Los Angeles nchini Marekani, kujibu tuhuma kuhusu namna matumizi ya mtandao hasa wa Instagram, unavyoathiri afya ya akili kwa watoto na vijana nchini humo.

Zuckerberg, amejitetea kuhusu madai ya kuwa matumizi ya Instagram, kwa vijana na watoto nchini Marekani, imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa magonjwa ya akili nchini Marekani.

Mtumiaji mmoja Mark Lanier, amekwenda Mahakamani kuishtaki kampuni hiyo baada ya matumizi ya Instagram na Youtube, kumsabababishia ugonjwa wa akili alipokuwa mdogo.

Mwanamke huyo anasema, mitandao hiyo miwili, ilimfanya kuwa na mawazo ya kujitoa uhai, lakini pia kupata msongo mkubwa wa mawazo.

Zuckerberg, anashtumiwa pia kwa kulipotosha bunge la Congress mwaka 2024 kwamba, muundo wa mitandao yake ya kijamii, haina athari kwa watuamiaji.

Iwapo mmiliki wa kampuni hiyo atapatikana na hatia kwenye kesi hiyo, atawalipa fidia watu wote waliothrika na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Katika hatua nyingine, kesi nyingine zaidi ya 1,600 zimefunguliwa nchini Marekani dhidi ya matumizi mengine ya mitandao ya kijamiii kama Tiktok, Google na Snap ambayo ripoti zinasema, inasababisha magonjwa ya akili hasa kwa vijana na watoto.

RFI