Kenya waruhusiwa kuandamana lakini wasiisogelee Ikulu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:40 PM Jun 27 2024
Maandamano Kenya.
Picha: Maktaba
Maandamano Kenya.

JESHI la Polisi nchini Kenya, limewataka waandamanaji katika eneo la Kisumu nchini humo kuendelea na maandamano yenye amani na kwamba wasithubutu kusogea katika viunga vya Ikulu.

Katika makubaliano hayo waliyoyaweka kati ya polisi wa Kisumu na waandamanaji, baadhi ya vijana wamekubaliana na rai hiyo na kusisitiza kwamba basi wapatiwe maji ya kunywa.

Vijana nchini Kenya wanaendelea na maandamano hii leo Juni 27 ambapo licha ya Rais Ruto hapo jana Juni 26, 2024, kukataa kuusaini Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 ambao ulikuwa ukipingwa, maandamano ya leo yanalenga kutoa shinikizo kwa Rais Ruto kujiuzulu.

Njia zote zinazoelekea Ikulu ya Kenya zimefungwa na Jeshi la Polisi nchini humo.