WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Israel, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ni marufuku kuingia nchi ya Israel.
Israel Katz, anasema uamuzi huo, unakuja baada ya Guterres kutolaani shambulio la kombora la Iran dhidi ya Israel, siku ya jana.
Anamshutumu mkuu huyo wa UN, kwa kuwa mpinzani wa Israel na kutoa msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji.
Guterres atakumbukwa kama doa katika historia ya Umoja wa Mataifa kwa vizazi vijavyo,” anaongeza Katz.
Jana, Jumanne, mkuu huyo wa UN, alilaani kuongezeka kwa mzozo wa Mashariki ya Kati na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.
BBC
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED