Serengeti Lite yazindua kampeni ya ‘Lite Your Imagination’ kuchochea ubunifu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:06 PM Nov 25 2024
Naibu Waziri wa Michezo,Hamis Mwinjuma, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Lite Your Imagination’ ya bia ya Serengeti Lite. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, Diamond Platnumz, balozi wa Serengeti, na Dk. Kedmon Mapana.
Picha:Mpigapicha Wetu
Naibu Waziri wa Michezo,Hamis Mwinjuma, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Lite Your Imagination’ ya bia ya Serengeti Lite. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, Diamond Platnumz, balozi wa Serengeti, na Dk. Kedmon Mapana.

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua kampeni ya ‘Lite Your Imagination’ chini ya bia yake ya Serengeti Lite. Kampeni hii inalenga kuhamasisha vijana wa Kitanzania kuibua vipaji vya ubunifu, kujieleza kwa uhuru, na kuboresha maisha yao kupitia ubunifu.

Uzinduzi wa kampeni hii uliofanyika jijini Dar es Salaam uliwakutanisha watu mashuhuri, waandishi wa maudhui, wanamuziki, na wateja kusherehekea ubunifu na uvumbuzi wa Kitanzania. Kampeni hii ya Serengeti Lite inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kutimiza ndoto zao, kuishi kwa ujasiri, na kusherehekea nyakati za furaha na hamasa.  

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi alisema, "Serengeti Lite si kinywaji tu cha kuburudisha; ni mtindo wa maisha unaosherehekea upekee wa jamii yetu. Kupitia kampeni hii, tunalenga kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kuibua vipaji vya ubunifu wao, kuishi kwa ujasiri, na kusherehekea nyakati za furaha. Hii ni ahadi yetu ya kuinua ari ya wateja wetu na kuwa sehemu ya safari yao ya ubunifu."  

Kaulimbiu ya kampeni hii, Lite Your Imagination, inahamasisha Watanzania kupata muamko kila wakati na kuutumia kufikia ndoto zao. Ladha na ubora wa Serengeti Lite inayoburudisha na msisitizo wake unaifanya bia hiyo kuwa chaguo namba moja kwa wale wanaopenda na kuthamini ubora katika burudani.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, alipongeza SBL kwa akisema, "Miradi kama hii inainua ari ya vijana wetu, ambao ndio taifa la kesho. ‘Lite Your Imagination’ inaendana na malengo yetu ya kitaifa ya kukuza sanaa, utamaduni, na uvumbuzi. Serengeti Lite si bidhaa tu; imekuwa jukwaa la kuhamasisha kujiamini na kushirikiana."  

Kama sehemu ya kampeni hii, Serengeti Lite imeshirikiana na msanii maarufu, Diamond Platnumz, ambaye safari na mafanikio yake yanaakisi kampeni hii. Ushirikiano na Diamond unaleta hamasa, ukionyesha uwezo usio na kikomo wa vipaji na ubunifu wa vijana wa kitanzania.