WAKULIMA nchini wamerahisishiwa huduma ya malipo ya mazao yao ambapo sasa watakuwa na uwezo wa kulipwa kwa mfumo wa kidigitali kupitia simu ya mikononi.
Kampuni ya huduma za simu ya mkononi ya Yas kupitia kitengo cha Mixx by Yas, imeahidi kuendelea kushirikiana na wakulima kupitia vyama vyao ushirika katika kutoa huduma hiyo.
Akizungumza kwenye hafla maalum mwishoni mwa wiki jijini Dodoma, Afisa Mkuu wa Mix by Yas, Angelica Pesha alisema kwa miaka saba, wamekuwa wakiwahudumia wakulima kupitia AMCOS, kuhakikisha malipo ya mazao yao yanafanyika kwa usalama na ufanisi kupitia mfumo wao wa kidijitali.
"Tutaendelea kushirikiana na vyama vya ushirika vya wakukima kuhakikisha malipo yao yanakuwa salama na yenye uhakika," alisema Angelica
Aidha alisema hadi sasa, Mixx by Yas imesaidia kusambaza zaidi ya Shilingi bilioni 110 kwa wakulima mbalimbali wa mazao kama korosho, ufuta, choroko, pamba na mtama kupitia vyama vya ushirika zaidi ya 500 nchini kote.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED