Makamu wa Rais wa Gambia awasili Tanzania

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:00 PM Jan 27 2025
Makamu wa Rais wa Gambia awasili Tanzania.
Picha:Mpigapicha Wetu
Makamu wa Rais wa Gambia awasili Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Gambia, Muhammad Jallow amewasili jijini Dar es Salaam ambapo anamwakilisha Rais Adama Barrow katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kuanza leo, Januari 27 na 28 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika  unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalodhamiria kuimarisha juhudi za pamoja za Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika katika kuhakikisha Afrika inaondokana na changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu.

Jallow amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Jumaa Aweso.