RAIS Félix Tshisekedi muda wowote anatarajiwa kuhutubia umma juu ya kile kinachoendelea Mashariki mwa DRC ambako yananaendelea mapigano makali yaliyosababisha kutwaliwa kwa Mji wa Goma na kundi la wapiganaji wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na jeshi la Rwanda.
Hotuba ya Rais Tshisekedi inatabiliwa kuwa na maazimio ya mkutano baina yake na viongozi muhimu wa kitaifa walioketi Mjini Kinshasa kujadili kadhia hiyo ya kuongezeka kwa mzozo katika mashariki ya DRC.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Vital Kamerhe ambaye pia alikuwepo katika mkutano huo, amethibitisha pasina kutaja siku na muda juu Rais Tshisekedi kutoa hotuba kuhusu mzozo uliopo katika taifa.
Watu 17 wametajwa kuuawa wakati mapigano hayo yanayoendelea kutikisa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) huku waasi wa M23 wakiendelea kukabiliwa na upinzani kutoka kwa jeshi na makundi ya waasi wanaounga mkono serikali.
Kadhalika Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao huku hospitali zikitajwa kukabiliwa na msongamano wa majeruhi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED