CRISTIANO Ronaldo ameongoza tena orodha ya wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani akiwa na mapato ya jumla ya dola milioni 260 mwaka 2024, kwa mujibu wa tovuti ya Sportico.
Wachezaji 100 wanaoongoza, wakitawaliwa na wachezaji kutoka mpira wa miguu, NBA, NFL, gofu na ndondi, walipata wastani wa dola bilioni 6.2 katika mapato ya jumla mwaka jana.
Idadi hiyo ni pamoja na dola bilioni 4.8 katika mshahara na fedha na zawadi, pamoja na dola bilioni 1.4 katika ridhaa.
Bingwa wa zamani wa tenisi wa Marekani, Coco Gauff ndiye mwamichezo wa kike aliyepata fedha nyingi zaidi mwaka jana akivuna na dola milioni 30.4.
Mkataba mzuri wa Ronaldo na Al Nassr ulimhakikishia kubaki kileleni kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuhamia Saudi Pro League Desemba mwaka 2022.
Sportico ilisema fowadi huyo wa Ureno, ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza umri wa miaka 40 wiki iliyopita, alipata mshahara mnono wa dola milioni 215.
Ronaldo yuko mbali sana na wanamichezo wengine duniani.
Nahodha wa Inter Miami na Argentina, Lionel Messi (dola milioni 135) anafuatia pamoja na fowadi wa Los Angeles Lakers, LeBron James (dola milioni 133.2).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED