Bingwa wa Nyonga na Magoti; Uzito unavyoathiri viungo hivyo

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:44 PM Feb 16 2025
Uzito mkubwa unaathiri nyonga, magoti
Picha: AI
Uzito mkubwa unaathiri nyonga, magoti

BINGWA Mbobezi wa Upandikizaji wa Nyonga na Magoti kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mlonganzila. Hamis, ameelezea kuhusu upandikizaji wa marejeo wa nyonga na magoti huku akionya uzito mkubwa huathiri mwenendo wa waliopatiwa huduma hiyo, hivyo waudhibiti.

Bingwa wa Nyonga na Magoti kutoka MNH-Mloganzila, Dk. Abubakar Hamis, alisema kutokana na waliofanyiwa huduma hiyo kufanyika wakati teknolojia ikiwa duni, ndio sababu ya kufanyiwa upasuaji wa marejeo.

Dk. Abubakar Hamis
“Baada ya miaka kadhaa kupitia vyuma hulegea, husagika katika maeneo vilikowekwa. Maambukizi pia ni sababu ya upasuaji wa marejeo, kidonda kinaweza kupata bakteria baada ya upasuaji.

“Mvunjiko palipowekwa kiungo au palipounganishwa ni sababu ya marejeo. Lakini zaidi ni uzito, uzito husababisha nyonga, magoti kusagika paliporekebishwa,” alisema bingwa huyo. 

Bingwa huyo amefafanua hayo jana, akieleza kuhusu kambi maalum Februari 26 hadi Machi 7, 2025.