Hasunga:Kula vizuri kunasaidia kuondoa msongo wa mawazo

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 05:36 PM Feb 16 2025
MBUNGE wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga
PICHA:MTANDAO
MBUNGE wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga

MBUNGE wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga amewataka Watanzania kula vizuri akisisitiza siyo anasa kama watu wanavyodhani bali ni sera ya kujenga uchumi.

Amesema hayo katika taarifa yake kwa waandishi aliyoitoa mtandaoni leo  huku akinukuu vitabu vya dini kwamba vinasema asiyefanya kazi na asile na kwamba msimamo wake kwa Watanznaia ni kufanya kazi kwa bidii na pale wanapopata wasisahau kula vizuri. 
“Kula vizuri kunasaidia kuondoa msongo wa mawazo baadala ya kufikiria kila wakati shida mbalimbali ukipata fedha weka bajeti kiasi kawekeze kingine nenda kale. " amesema Hasunga.
“Ninawapongeza sana Watanzania katika maeneo mengi wameitekeleza hii sera na maeneo mengi uchumi umeanza kukua na kuchangamka kwa sababu kuna mzunguko mkubwa wa fedha. 
“Maaeneo ambayo watu hawali maisha uchumi uko chini mimi ninawasisitiza kuleni maisha, mimi ninawasisitiza watanzania wafanye kazi kwa bidii lakini tukipata tule vizuri” amesema Hasunga.