Chino aipeperusha Bendera ya Tanzania kwa ushindi wa Mkanda wa IBA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:55 AM Dec 27 2024
Chino aipeperusha Bendera  ya Tanzania kwa ushindi  wa Mkanda wa IBA
Picha:Mpigapicha Wetu
Chino aipeperusha Bendera ya Tanzania kwa ushindi wa Mkanda wa IBA

BONDIA Mtanzania Said Chino anaungana na Mabondia wengine wa Tanzania kwa kuweza kuipeperusha Bendera ya Tanzania kwenye pambano la kutetea mkanda wa International Boxing Association Inter-continental lightweight championship (IBA Inter-continental) baada ya kumpasua Bondia kutoka Afrika Kusini Malcolm Klassen kwa pointi za majaji wote watatu.

Chino ameshinda pambano hilo la Raundi 10 lililopigwa usiku wa kuamkia leo Desmba 27,2024 kwenye Ukumbi wa Super Dome Masaki, ambapo Jaji namba moja ametoa pointi 99 kwa 91 Jaji namba mbili ametoa pointi 100 kwa 90 na Jaji namba tatu ametoa pointi 99 kwa 91.

Kwa ushindi huo, Said Chino ameubakisha mkanda wake wa IBA Tanzania na anaondoka na  #KnockoutYaMama ya shilingi milioni tano kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

#KnockoutYaMama

1