"Wanaopiga kelele kuchaguliwa kwa Rais Samia wakapige kwenye vyama vyao"

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 06:13 PM Feb 19 2025
MBUNGE wa Arusha Mjini Mrisho Gambo.

MBUNGE wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) na wanachama wake wameshafanya maamuzi ya kumteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais hivyo wanaopiga kelele wanapaswa kukaa kimya kwa sababu wao sio wanachama wa chama hicho.