Tusiharibu Vyanzo vya Maji, ndiyo uhai wetu- Rais Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:36 PM Sep 24 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Mnakumbuka wakati wa kampeni, tuliahidi kumtua ndoo mama kichwani. Sasa tumekwenda kuifanyia kazi ahadi ile. Tumeifanyia kazi kwa kusambaza miradi ya maji nchi nzima. Kama mnavyoona tulivyofanya Ruvuma na nchi nzima ni hivyo hivyo. Kwa hiyo tunatarajia ikifika mwaka kesho 2025 tuwe tumetimiza lile lengo tulilotumwa na Chama Cha Mapinduzi kwamba vijiji vyote vya Tanzania vipate maji kwa asilimia 85 tutakuwa tumelitimiza au kupita kidogo,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.