SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limeongeza safari za treni la daladala maarufu ‘Mwakyembe’, kutokana na mahitaji ya usafiri kwa siku mbili, kuingia na kutoka mjini kati, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Fredy Mwanjala, alisema hayo kwenye taarifa yake, kwa umma, akisema hatua hiyo inatokana na kufungwa barabara za kuingia katikati ya jiji.
Alisema kufungwa kwa barabara hizo kutokana na mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika, ulioanza leo, Januari 27, 2025.“Treni zilizoongezwa ni ya saa 12: 00 asubuhi kutoka Stesheni ya Kamata (Gerezani) na treni ya saa 12: 00 jioni kutoka Pugu Stesheni.”
Safari hizo ni kwa ajili ya siku mbili, Januari 27 na 28, mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED