"RAIS Samia Suluhu Hassan ametuagiza viongozi wote kwenda kuwatumikia wananchi katika maeneo ambayo tumekabidhiwa dhamana hii, ikiwemo kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi," amesema Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi.
Kihongosi ameyasema hayo leo baada ya kuanza rasmi ziara ya kutembelea vijiji vya Nyamikoma, Mwandama, Sapiwi, Igegu Magharibi,Igegu Mashariki, Igegu, Isenge, Mwamabu, Igagalulwa, Sengerema na Majengo.
Amesema yuko tayari kwenda katika vijiji na kusikiliza changamoto zinazowakabili maana kupitia wananchi ndio watakaoibua matatizo mbalimbali, pamoja na kero zinazowakabili.
"Hiyo pia itasaidia kujua wapi pana shida ikiwemo ukosefu wa huduma muhimu kama umeme, maji, afya, elimu, pembejeo na hata miundombinu korofi ya barabara," amesema Kihongosi.
"Maendeleo ya watu katika mikoa, wilaya, vijiji na hata vitongoji, kwa kuliona hilo ndio maana nimeanza ziara ya siku 30 kwenda kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi katika vijiji vyote vya mkoa wa Simiyu," amesema Kihongosi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED