JESHI la polisi limezuia kufanyika kwa mkutano kati ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika.
Mkutano huo ulikuwa ufanyike leo saa tano asubuhi katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Mikocheni mkoani Dar es Salaam, lakini saa chache kabla ya tukio Jeshi la polisi lilizingira eneo hilo na kuanza kuwazuia waandishi wa habari waliokuwa wanaingia katika ofisi hizo.
Hata hivyo, alipotafutwa Mnyika na Nipashe Digital kujua iwapo kuna sababu maalumu imetolewa na jeshi hilo amesema “Hawajampa taarifa yoyote ya kwanini wanazuia mkutano huo. Hawajaonana na mimi wala kuwasiliana kueleza sababu” amesema Mnyika
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED