Nishati safi ni mwito wa kuokoa maisha na mazingira

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 03:16 PM Jan 11 2025
Ofisa Nishati Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, Mussa Abbas.
Picha: Mpigapicha Wetu
Ofisa Nishati Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, Mussa Abbas.

OFISA Nishati Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, Mussa Abbas, zaidi ya watu 33,000 hufariki kila mwaka nchini kwasababu ya matumizi ya nishari chafu hivyo hamasa ya matumizi ya nishari safi inafanyika mahususi kwaajili ya kuokoa maisha wa watanzania na mazingira kwa ujumla.

Pia amesisitiza umuhimu wa elimu na rasilimali ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Akibainisha kwamba takribani asilimia 82 ya Watanzania hutegemea tungamo taka kama kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia, hali inayochangia madhara makubwa ya kiafya, kimazingira, na kijamii.

Abbas ameyasema hayo leo Jumamosi, Januari 11, 2025 katika hafla maalumu ya uhamasishaji na kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia kwa viongozi wa dini ya Kiislam Jijini Arusha, ambayo imeratibowa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

"Watu takriban bilioni 2.3 duniani bado hawajafanikiwa kutumia nishati safi ya kupikia huku chini ya Jangwa la Sahara kwa Afrika wakiwa watu milioni 990.



"Takribani watu milioni 3 dunia nzima huwa wanafariki kwa magonjwa ya hewa ambayo yanatokana na matumizi ya nishati chafu, pia kati ya hao takribani asilimia 60 ni wanawake na watoto, na kwa Afrika pekee takribani watu 400,000 hado 700,000 hufariki kutokana na madhara yanayosababishwa na nishati chafu, kwa Tanzania watu 33,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo hayo," ameeleza Abbas.

Amesema Wizara ya Nishati ina Sera ya Nishati ya mwaka 2015 ambayo imeweka bayana kwamba Tanzania inatakiwa kutoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa kwenda kwenye nishati safi.

Aidha, ameeleza kuwa sera hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuwezesha utekelezaji wa matumizi ya nishati safi.