Kambi ya Mtoto Vunja Ukimya yaibua kesi 856 za ukatili dhidi yao

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 05:33 PM Nov 18 2024
 Kambi ya Mtoto Vunja Ukimya yaibua kesi 856 za ukatili dhidi yao.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kambi ya Mtoto Vunja Ukimya yaibua kesi 856 za ukatili dhidi yao.

KAMBI ya siku tano katika Shule za Msingi kutoka Kata ya Manzese na Kwembe Manispaa ya Ubungo iliyopewa jina la Mtoto Vunja Ukimya imeibua kesi 856 kati ya hizo 597 zimetokana na unyanyasaji wa kingono na 259 zimetokana na kesi za kifamilia.

Katika kesi za unyanyasi wa kingono dhidi ya watoto, 80 zilikuwa ni za ubakaji, 69 za ulawiti na 448 zilitokana na shambulio la aibu zote dhidi ya watoto.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Shirika la Macho kwa Jamii,Thelesia Lihanjala alisema kuwa wameweza kuibua kesi hizo zote zitokanazo na changamoto zinazowakabili watoto ambazo walikuwa nazo vifuani mwao ambazo hawakuweza kuzisemea kokote.

Alisema kambi hiyo ilikuwa ni ya siku tano walitembelea katika shule tano za msingi kutoka manispaa hiyo ambapo alisema katika kesi hizo 401 zilihusisha wanaume na kesi 455 zilihusisha wanawake.

Lihanjala alibainisha kesi za kingono dhidi ya watoto katika manispaa hiyo bado ni tishio kwakuwa watoto wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za ukatili wa kingono kutoka majumbani na walikuwa hawajui pa kusemea kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Alisema katika kambi hiyo waliweza kuwapa watoto elimu na mbinu stahiki kuwahi kusema changamoto zao kabla hawajaathirika zaidi na vitendo hivyo vibaya dhidi yao kwakuwa kesi nyingi walizozibaini na kuziibua tayari mtoto wameshaharibikana kuathirika.

Chati.

Hata hivyo aliomba vyombo husika vya usalama, haki na watetezi dhidi ya watoto kushirikiana kwa pamoja kusimamia na kuziendesha kesi hizo walizoziibua na ili kutokomeza vitendo hivyo wakiwemo waendesha mashitaka, watu wa ustawi, mawakili.

Naye Stella Charles Afisa Ustawi Jamii Manispaa ya Ubungo alisema kambi hizo zilizoandaliwa na Shirika hilo kwa kuwezeshwa na THRDC,LHRDC na Save the Children zimewasaidia watoto kuvunja ukimnya na kuweka wazi kufunguka changamoto zao zinazowakabili ambapo awali walikuwa hawajagundua changamoto hizo.

“Kwakweli hili shirika tunaishukuru sana kwambinu ao kuweka kambi na kuongea na watotokwa ukaribu imetsaidia kutuzinua masikiona kubaini changamoto nyingi sana dhidi ya watoto, sasa tutakijikita na kufatilia kesi hizo na kuwashughulikia wale wote wanaofanya vitendo viovu kwa watoto wetu” alisema

Hata hivyo amewataka wazazi wawe karibu na watoto watenge muda kuwadososa watoto wao ili wajue changamoto zinazowapitia watotokwakwua watoto hao wanaathirika kupitia ndugu wa karibu na kuwataka wazazi kutokuwaamini ndugu wa karibu kwakuwa kambi zimebaini watoto wengi hawanaathiriwa na watu wa karibu.

Alisema kambi hizo zimebaini  wazazi wengi wamekuwa wakikosa muda wa kuwa karibu na watoto wao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa upendo kwa watoto na hata ukali uliopitiliza kwa watoto.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa alisema watahakikisha wanasimama kusimamia haki na utu wa watoto unaheshimiwa nchini.

“Tutasimamia ha kutetea haki za watoto hadi tone la mwisho tutahakikisha wale wote waliohusika kufanya vitendo viovu dhidi ya watoto watachukuliwa hatua ili kuweza kukomesha vitendo hivyo” Olengurumwa