TAASISI ya vyombo vya habari kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania(MISA-TAN),imepata Mwenyekiti mpya wa Taasisi hiyo Edwin Soko, na kuchukua mikoba ya Salome Kitomari ambaye alikuwa mwenyekiti kwa taasisi hiyo kwa muda wa miaka 8.
Uchaguzi huo umefanyika leo Novemba 4,2024, ukisimamiwa na Mwenyekiti wa uchaguzi Ali Aboth, ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 46.
Aboht akitangaza matokeo hayo,amemtangaza Edwin Soko kwa Mwenyekiti mpya wa Misa -Tan kwa kupata kura 33,akifuatiwa na Said Mmanga,kwa kupata kura 9, nafasi ya tatu Betty Masanja aliyepata kura 3, huku kura moja ikiharibika.
Ametangaza wajumbe wa Bodi ya Misa-Tan,ambao wameshinda, kuwa ni Prosper Kwigize aliyepata kura 31, akifuatiwa na Alex Benson Sichona aliyepata kura 28.
Ambapo nafasi hiyo ya wajumbe walikuwa wakishindania watu watano, akiwamo Othman Maalim aliyepata kura 15, akifuatiwa na Izack Wakuganda kwa kupata kura 8,na Juma Mdimi naye alipata kura 8 huku kura moja ikiharibika.
Aidha,aliyekuwa Mwenyekiti wa Misa-Tan Salome Kitomari,ameishauri bodi hiyo mpya,kwamba waendeshe taasisi hiyo kwa kuzingatia Katiba.
Naye Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Misa-Tan Edwin Soko,ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,na kuahidi mambo makubwa ikiwamo kuiendeleza na kuikuza, huku akiomba pia ushirikiano wa kutosha kwa wanachama.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED