Wakili Peter Madeleka ameandika kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) “Kwa mujibu wa taarifa niliyopewa muda mfupi uliopita na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ni kwamba, Dkt. Wilbrod Slaa ataendelea kusota magereza hadi Januari 30, 2025, kwa sababu “Kuna ugeni wa marais.”
Ameendelea “Haki kwa mahabusu gerezani, Kitendo cha Mahakama kushindwa kutoa huduma kwa sababu ya “Ugeni wa Marais” ni kuwatesa mahabusu. Naomba Mahakama Mtandao itumike ili kuwatendea haki watu waliopo magerezani.”
Madeleka na Jopo la Mawakili wanaomwakilisha Mwanasiasa huyo katika Kesi ya Jinai Namba 993 ya Mwaka 2025, waliwasilisha maombi Mawili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, kupinga kunyimwa dhamana kwa mteja wao na kupinga uhalali wa kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED