ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, Ester Mahawe, amezikwa leo na maelfu ya watu nyumbani kwake Ngaramtoni ya chini jijini Arusha,huku akimwagiwa sifa za kuwa mstari wa mbele kwa utetezi wa wanaume.
Ester, alifariki Januari 14 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro na kuacha mume na watoto watatu na watoto sita wa kuwalea pamoja na wajukuu tisa.
Marehemu alifariki akiwa anarudi Arusha Januari 13 mwaka huu kutoka Hospitali ya Lugalo Dar es Salaam na akiwa njian hali yake ilibadilika na kulazimika kupelekwa Hospitali ya KCMC ambako alifariki.
Akizungumza jana kwenye ibada ya mazishi ya Ester, Ngaramtoni ya Chini jijini Arusha, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange, ametoa pole kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, huku akiwasihi wengine kuacha hadithi iliyo njema kama aliyoiacha ya utetezi wa wanaume.
"Marehemu anasifa nyingi ila mwinyi alishasema maisha ya mwanadamu ni hadithi tu, ila jitahidi kuwa hadithi iliyo njema ili wanaobaki waendelee kuyasimulia, huyu ndugu yetu Ester ametuachia hadithi njema ya kuwatetea wanaume na kuacha upendo kwa kila mtu,"amesema.
Amesema alifanya kazi kwa ufanisi na kuwa mfano bora kwa wenzake waliopewa nafasi na Rais, hivyo kila mmoja ahakikishe anabaki kuwa hadithi iliyo njema kwa wale anaowaongoza.
"Kila dhamana mnayopewa muifanyie kazi kwa bidii na maarifa ya hali ya juu hilo ndilo aliloliacha marehemu na alisisitiza hata mwanamke ukipata V8 hesimu mwanaume,amesema
Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema Ester ametutoka lakini ameacha sifa nyingi na kila mmoja anayemfahamu anacho cha kumwelezea juu ya ucheshi, upendo na kuheshimu mkubwa na mdogo bila kujali washifa wake.
"Mimi ni mzee wa Mkoa wa Manyara Ester namfahamu vizuri ila sijawahi kumuona akija nisalimia akiwa amekasirika, hata kama ameudhiwa atakusalimia akiwa anafurahi hatakasiriki hovyo hovyo, lakini mchapakazi sana.
"Lakini alikuwa mtetezi wa wanaume ila juna baadhi ya wamama wakiongea utafikiri tunaonea sana wanawake, lakini Ester alikuwa anatutetea sana na alikua akiwasema akna mama wenzake na kusema hawa watu wanaoitwa wanaume muhimu sana lazima tukae nao vizuri na lazima tuwatunze hasa nyie wakubwa mkipewa V8 hamfui nguo zao, mnaanza kuwanyanyasa wanaume hakika nin wanawake wachache wanaosema haya,"amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, ametoa pole kwa wafiwa na kusema alikuwa mtumishi na rafiki yao waliyofanya naye kazi pamoja na ushirikiano mkubwa.
"Sisi kule Songwe tunafanya kazi kama timu hizi dhamana zinapita tukipendana, tukishirikiana mengine yote ni ziada mwenyezi mungu hatupi dhamana iwe fimbo kwa wengine bali anatupa kama daraja la kuvusha wengine na hili Ester aliliishi kwa matendo,"amesema.
Amesema marehemu anaheshima ya kuwa balozi na mtetezi wa kweli wa wanaume ,na wengi wameshuhudia hilo wazi wazi na ameacha deni kwa wakuu wa wilaya na hasa akna mama kua kuna nafasi ya kusema ukweli alafu mambo yako yakuonyokee na kusemwa milele.
Aidha amesema sasa hivi kuna janga kubwa la watoto wa kiume, tunawajibu wa kuwasemea watoto wa kume ili makuzi yao yaendane na msingi na tukifanya mchezo tutakua na janga na kizazi kilichohaharibika.
Tumekua na harakati nyingi za kumpigania mtoto wa kike na kuwasahau watoto wa kiume, jambo ambalo si sawa.
Mwenyekiti wa wakuu wilaya na Mkuu Wilaya mwanga, Mwanahamisi Kila tulipomkimbilia anakupa ushauri na kuwapa elimu juu ya uongozi.
Mshauri wa Rais Ofisi ya Rais masuala ya wanawake, Angela Kairuki ametoa pole kwa niaba ya rais, lakini Taifa limepata pigo na familia imepata pigo kwa kuondokewa na Ester.
"Mimi binafsi niliongea naye Christmas akiwa amepanga mengi na alionyesha kupambana lakini ameondoka,tutamkumbuka alifanya mengi sana na ameacha alama,"amesema.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa akna mama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Zanainabu Shomari, alijali Taifa lake kuliko hata afya yake aliporudi katika matibabu ila siwezi pumzika sababu ninakazi kubwa naenda kushiriki.
"Sisi akna mama CCM tumepoteza mwanamke shujaa na mwenye nidhamu ya kuheshimu wenzake na alipenda watu na kazi yake,"amesema.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Misaille Mussa, akiongea kwa niaba ya Mkuu Mkoa Arusha Paul Makonda ametoa pole za makamu wa Rais Philip Mpango.
Akisoma wasifu wa marehemu mtoto wa marehemu Lulu Alexander amesema marehemu alipata changamoto ya maradhi ya saratani Agosti mwaka 2023 ambapo alipata huduma za matibabu katika Hospitali ya Apolo nchini India,Ocean Road,Muhimbili,Lugalo zilizopo Jijini Dar es salaam na hatimaye KCMC mkoani Kilimanjaro.
Amesema enzi za uhai wa mama yake Ester, alichaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Manyara mwaka 2015 hadi 2020 na pia mwaka huo alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa mkoa wa Manyara.
Aidha amesema mwaka 2021 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa amkutano Mkuu wa CCM Taifa na Juni 2021 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na mwaka 2023 alihamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo aliudumu hadi mauti yalipomfika.
Pia amesema mwaka 2012 marehemu alianzisha shule yake ya mchepuo wa kiingereza ya Intel iliyopo jijini Arusha, ambayo kwa sasa inatoa elimu ya awali, Msingi na Sekondari.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED