CWT-Watumishi wanaoshughulikia maslahi ya walimu wanatusumbua

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 03:41 PM Feb 13 2025
Makamu wa Rais wa CWT Taifa, Suleiman Ikomba.
Picha: Mpigapicha Wetu
Makamu wa Rais wa CWT Taifa, Suleiman Ikomba.

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimeitaka serikali kuwachukulia hatua ikiwezekana kuwaondoka katika nafasi zao watumishi wanaoshughulikia maslahi ya walimu kwasababu wameshindwa kutenda kazi zao vizuri na kusababisha walimu kuwa na msongo wa mawazo.

Makamu wa Rais wa CWT Taifa, Suleiman Ikomba, ametoa tamko hilo jana Februari 12, 2025  wakati wa mkutano wa kutatua changamoto za walimu wa Mkoa wa Singida katika kliniki ya ‘Samia Teachers Mobile Clinic’ iliyoratibiwa na CWT kwa kushirikiana na Ofisi ya Raisa Utumishi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Wizara ya Elimu na Tume ya Utumishi Tanzania mamia ya walimu kutoka halmashauri saba za Mkoa wa Singida wamefika mjini Singida kuwasilisha madai yao ambayo wanadai kwa muda mrefu ili yatatuliwe.

“Hawa watumishi ambao wanashughulika na maslahi yetu walimu tumejikuta wanatusumbua sana, tunaomba wanaotusumbua waache kutusumbua kwasababu mwisho wa siku tunataka tuanze kuchukua hatua kwa mtu kwa jina sio kwa kuichafua serikali,”alisema.

1