Kihenzile akaribisha wawekezaji sekta ya usafirishaji.

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:53 PM Nov 13 2024
Naibu Waziri Wa Uchukuzi, David Kihenzile
Picha: Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Wa Uchukuzi, David Kihenzile

SERIKALI imetenga zaidi ya trilioni moja kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Meli katika ziwa Tanyanyika na Ziwa Victoria ili kuwezesha huduma ya usafiri na usafirishaji kuwa bora katika maziwa hayo.

Hayo yamesemwa jiiiji Dar es Salaam na Naibu wa Uchukuzi Davidi Kihenzile wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa magari ya kampuni ya Foton kutoka China.

“Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya uchukuzi ili  kurahisha usafirishaji  mizigo na abiria wa  ndani na nje ya nchi hivyo ujio wa kampuni hii ya Foton itasidia sana kukuza sekta hii ya usafirishaji” Alisema Kihenzile.

Pia Naibu Waziri Kihenzile  ametoa wito  wawekezaji wa Sekta ya Usafiri na Usafirishaji kuendelea kuwekeza Tanzania kutokana na amani na Mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya Sita.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Kampuni Foton Hanif Salamha amesema kuwa  kwa sasa wamefungua ofisi katika nchi za Tanzania, Kenya,Uganda , Angola na Mozambique  hivyo kufanya huduma hiyo kuwa bora kwa watumiaji.

Aidha, Hanifa amesema kuwa kwa Tanzania wanategemea kufungua  ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mafinga, Songea, Babati, Majimoto  na Kahama.

Kampuni ya Foton imetambulisha Magari yenye uwezo  kubeba  kuanzia tani kumi mpaka tani 1.9.