Zitto: CCM inawabebesha wakulima ushuru kinyume na sheria Mbeya

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:35 PM Sep 23 2024
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Picha:Mpigapicha Wetu
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe

Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekemea utozwaji wa ushuru wa mazao ya wakulima kinyume na sheria na kutoa wito kwa wananchi kuchagua upinzani ili kuondoa unyanyasaji unaofanywa na Serikali za Halmashauri za Kyelwa, Rungwe, Lupa mkoani Mbeya.

Akizungumza na wananchi wa Kyelwa mwishoni mwa wiki alisema; "Wakulima wanyanyaswa sana huku (Mbeya), mkulima akitoa mpunga wake shambani akiupeleka nyumbani kwanza anatozwa gunia Shilingi 2,000. Akiutoa nyumbani na kuupeleka mashineni anatozwa gunia shilingi 2,000. Kwanini mkulima atozwe kwakutoa mazao yake shambani. Mkulima anapaswa kutozwa wakati wa kuuza. Kodi haikusanywi kwa mtu, kodi inakusanywa kwa muamala wa kibiashara." alisema Zitto

Katika hatua nyingine, alitaka wananchi kufanya maamuzi kwa kuchagua upinzani.

"Dawa ya kuondokana na mzigo huu wa ushuru ni kuweka Halmashauri ya Wilaya ambayo inaongozwa na vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo. Tushirikiane tuondokane na hizi, ushuru ambao kwanza kinyume na sheria lakini pili unawanyonya wananchi"

Zitto yupo katika ziara ya Chama ya viongozi wakuu nchi nzima inayolenga kuyafikia majimbo yote 214 ili kuwasikiliza wananchi, kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusajili wanachama milioni 10 kwa miezi 10.