PSSSF yatoa huduma Wiki ya Utamaduni wa Mtanzania Songea

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:13 PM Sep 23 2024
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Yessaya Mwakifulefule (kulia) akimhudumia Mwanachama aliyefika katika banda la PSSSF, katika maonesho ya Wiki ya Utamaduni wa Mtanzania yanayoendelea Songea mjini,mkoani Ruvuma. PSSSF ni moja ya wadhamini.
Picha:Mpigapicha Wetu

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF unashiriki Maonesho ya Wiki ya Utamaduni wa Mtanzania yanayoendelea katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

2

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Yessaya Mwakifulefule (kulia) akimhudumia Mwanachama aliyefika katika banda la PSSSF, katika maonesho ya Wiki ya Utamaduni wa Mtanzania yanayoendelea katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Maonesho hayo yanakwenda sanjari na Tamasha hilo ambalo lilizinduliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ambaye aliwaasa watanzania kuzingatia miiko, mila na desturi za kitanzania na kuwarithisha watoto na vijana ili kujiepusha na tamaduni za kigeni zisizofaa kwa jamii.

Tamasha hilo linatarajiwa kifikia kilele leo Septemba 23, 2024 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.