Yas, Samsung wazindua simu zenye AI

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 07:59 PM Feb 18 2025
Yas, Samsung wazindua simu zenye AI.
Picha: Mpigapicha Wetu
Yas, Samsung wazindua simu zenye AI.

KATIKA kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia. Kampuni ya Yas kwa kushirikiana na Samsung leo wamezindua simu mpya ya Galaxy S 25 Series.

Alizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hizo jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Huduma za ziada wa Yas, Ikunda Ngowi, alisema uzinduzi wa simu hizo ni katika kuwaweka watanzania karibu teknolojia mpya ya akili mnemba (AI) ambazo zinapatikana kwenye simu hizo.

"Leo tunazindua ushirikiano wetu na Samsung,  wateja wafurahie ubora wa teknolojia yetu, na utendaji kazi wa Artificial Interagency, AI (akili mnembe)," alisema Ikunda.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha biashara za simu wa Samsung, Ngobe Kiwanga, alisema kampuni hiyo inafurahia ushirikiano wao na Yas unaoleta manufaa kwa watanzania.

1