TIB, SIDO wawanoa wafanyabiashara

By Jumanne Juma , Nipashe
Published at 04:50 PM Nov 16 2024
Ofisa mikopo wa Benki ya TIB, Eugen Ingwe, akizungumza na
wajasiliamali wadogo na waka kati kwenye Semina ya Siku Moja
iliyoandaliwa na Shirika la Viwanda vidogo (SIDO), na uhirikiano wa benki hiyo katika kuwajengea uwezo na kuwaelekeza fursa za mikopo.
Picha:Jumanne Juma
Ofisa mikopo wa Benki ya TIB, Eugen Ingwe, akizungumza na wajasiliamali wadogo na waka kati kwenye Semina ya Siku Moja iliyoandaliwa na Shirika la Viwanda vidogo (SIDO), na uhirikiano wa benki hiyo katika kuwajengea uwezo na kuwaelekeza fursa za mikopo.

Benki ya Maendeleo (TIB) kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) chini ya usimamizi wa Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Hopeness Elia wameendesha warsha fupi kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo waliolelewa na kukuzwa na Shirika la SIDO juu ya fursa za mikopo nafuu ya wajasiriamali ipatikanayo katika Benki ya Maendeleo TIB.


Warsha hiyo imefanyika Jijini Dar es salaam  iliyohudhuriwa na wafanyabiashara wapatao 40 kutoka zekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Viwanda, Kilimo, Ujenzi, Usafirishaji wa bidhaa nje nchi, na Afya.

Mwakilishi wa Meneja wa TIB Kanda ya Dar es Salaam Eugene Naftal Ingwe amesema Benki ya TIB iko tayari kusikiliza mawazo yao na kuwashauri kitaalamu kwani Benki hiyo inakitengo maalumu cha wataalamu wa majengo na ufundi wa miradi.

Ameendelea kwa kuwafafanulia wajasiriamali hao kuwa wakisha kamilisha vigezo vyote vinavyotakiwa watawatembelea katika miradi yao na mengine yataendelea kulingana na miradi yao ilivyo kwa kuwa Benki hiyo ya TIB  ina fursa mbalimbali za mikopo ya SME ipatikanayo katika Benki hiyo.

Mkurugenzi wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO), Hopeness Elia, akizungumza na wajasiliamali wadogo na waka Kati kwenye Semina ya Siku Moja katika kuwajengea Uwezo na kuwaelekeza fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya (TIB), kupitia dirisha dogo la uwekezaji nchini jijini Dar es Salaam jana kulia ni Ofisa mikopo wa benki hiyo, Eugen Ingwe. PICHA: JUMANNE JUMA