HALMASHAURI ya Wilaya ya Singida imekumbushia ahadi ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi ya kujengewa soko la vitunguu ambalo litasaidia kuongeza mapato ya halmashauri ambapo imeiomba serikali kutoa Sh.bilioni 2 ili kufanikisha ujenzi wa soko hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida,Elia Digha, akizungumza leo Februari 13,2025 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo amesema Dk.Nchimbi akiwa katika ziara Mei mwaka jana mkoani Singida aliahidi serikali itajenga soko la vitunguu kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula, amesema halmashauri imeweka makadirio ya mpango wa bajeti ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ya Sh.bilioni 36.5.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED