Bosi PSSSF: Tuko Sabasaba kuunga mkono juhudi za serikali katika biashara na uwekezaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:34 AM Jul 03 2024
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul-Razaq Badru akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya Sabasaba
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul-Razaq Badru akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya Sabasaba

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul-Razaq Badru, amesema Mfuko huo unashiriki katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ili kutoa huduma kwa wananchama wake lakini pia kuunga mkono jitihada za serikali katika eneo la biashara na uwekezaji.

1Badru ameyasema hayo Jana Julai 2, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo kuhusu ushiriki wa PSSSF kwenye Maonesho hayo.

“Pamoja na kutoa huduma za wanachama pia tunawekeza katika maeneo mbalimbali, na kama kaulimbiu inavyosema, Tanzania ni Sehemu Salama kwa Biashara na Uwekjezaji, na sisi PSSSF tuko hapa kwenye Maonesho haya ili kuwaeleza wanachama na wananchi kwa ujumla fursa zilizopo katika uwekezaji uliofanywa na Mfuko, tumewekeza kwenye majengo ya kupangisha ofisi,maduka, migahawa, nyumba za bei nafuu lakini pia viwanja kwa wale wenye uhitaji.” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul-Razaq Badru akimpa zawadi mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya Sabasaba
Aidha kuhusu maboresho ya utoaji huduma, Badru amesema, Mfuko umejidhatiti kuhakikisha unaachama nna matumizi ya karatasi na badala yake umeelekeza nguvu zake kuwaelimisha wanachama wake matumizi ya huduma kupitia mtandao PSSSF Kidijitali.

Tunatumia fursa ya maonesho haya, kuwaelimisha wanachama wetu jinsi ya kutumia PSSSF Kiganjani Mobile App, ambayo inasahisisha utoaji wa huduma na kupunguza gharama, amesema.

Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2024 yatafikia kilele Julai 13 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Julai 3, na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi.