REAL Madrid, wako tayari kuongeza kasi ya kumsaka beki wa pembeni wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, huku Los Blancos wakiwa na uhakika wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 26.
Mkufunzi wa Al-Hilal Jorge Jesus anataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah msimu huu wa joto, huku Mmisri huyo mwenye umri wa miaka 32 akikataa kandarasi mwishoni mwa msimu.
Lakini matumaini ya kumsajili Salah kutoka Liverpool yanafifia miongoni mwa klabu za Saudi Arabia, ambazo zinahisi vinatumiwa kama mwafaka katika mazungumzo ya kandarasi.
Liverpool inasisitiza kuwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, hauzwi licha ya kutakiwa na Saudi Pro-League. (Mail – Subscription Required), Arsenal ndio wana uwezekano mkubwa wa kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED