Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, John Healy amesema hakuwezi kuwa na mazungumzo kuhusu Ukraine bila kuishirikisha Ukraine yenyewe katika mazungumzo hayo.
Waziri huyo wa Uingereza amesema hayo wakati wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Nato mjini Brussels.
Akijibu maoni ya Donald Trump kuhusu vita vya Ukraine hapo jana, anasema kazi ya Nato ni kuiweka Ukraine katika nafasi imara zaidi kwa mazungumzo yoyote yajayo.
Healey pia amesema kutakuwa na matangazo mapya ya kuiunga mkono Ukraine kupitia Nato, huku mabilioni ya silaha mpya za wapiganaji wa Ukraine zikiwa mstari wa mbele.
"Tunataka kuona amani ya kudumu na hakuna kurudi kwa migogoro na uchokozi na tusisahau Urusi bado ni tishio zaidi ya Ukraine." Amesema
Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine ndani ya kipindi cha saa 24 kwa njia ya mazungumzo lakini hadi sasa hakuna kilichowekwa wazi katika mkakati huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED