Halmashauri Mkalama yawajaza mamilioni wanawake, vijana na walemavu

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 03:04 PM Feb 13 2025
 Halmashauri Mkalama yawajaza mamilioni wanawake, vijana na walemavu.
Picha: Mpigapicha Wetu
Halmashauri Mkalama yawajaza mamilioni wanawake, vijana na walemavu.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imekabidhi mikopo ya Sh.milioni 395 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Asia Messos,akizungumza jana wakati wa hafla ya kutoa mikopo hiyo alisema baada ya dirisha kufunguliwa jumla ya vikundi 143 vilituma maombi ambapo vikundi 73 vimefanikiwa kupata mikopo hiyo katika awamu ya kwanza ambapo katika vikundi hivyo vilivyopata mkopo vya wanawake 51, vijana 19 na vikundi 3 vya watu wenye ulemavu. 

Naye Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alitoa  wito kwa vijana, wanawake na watu wenye ulevamavu wilayani Mkalama kutumia vizuri mikopo wanayopewa kwa kuwekeza katika biashara zenye tija ili waweze kujikwamua kiuchumi na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.