KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, alikuwa mmoja wa wachezaji walioanza kwenye mchezo kati ya timu hiyo dhidi ya Singida Black Stars, uliochezwa, Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja tu baada ya kufunga ndoa na mwanamitindo maarufu nchini, mwigizaji na mjasiliamali, Hamisa Mobeto.
Aziz Ki, alicheza mchezo huo, huku akishangaza wengi kwa kucheza kwa kiwango kile kile, akipiga mashuti kadhaa langoni wa Singida, ingawa hakuwa na bahati ya kupata bao.
Wengi walishazwa naye kwa kucheza mchezo huo, ambapo walidhani kwamba anaweza kuwa mapumzikoni leo, au fungate, ' akila bata' na mwenza wake, lakini alikuwa uwanjani kuitetea timu yake ya Yanga ambayo alichangia ushindi wa mabao 2-1.
Alifanya majaribio kadhaa dakika ya pili, alipopata pasi kutoka kwa Maxi Nzengeli, akapiga mpira juu.
Dakika ya sita, Aziz Ki, kwa mara nyingine tena, alikosa bao la wazi, baada ya shuti lake la chini kutoka nje sentimeta chache mpira ukiwa umeshampira kipa, Hussein Masalanga.
Kipindi cha pili, alipata nafasi moja ya kupiga shuti kali lilikiwababatiza mabeki wa Singida, kabla ya kuwahiwa na kipa Masalanga.
Ndoa ya mchezaji hiyo, raia wa Burkina Faso, ilikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari kabla na siku ya kufunga ndoa, huku pia ikiendelea kutikisa mitandao ya kijamii.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED