Nyota chipukizi wa kuwatazama Euro 2024

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:43 AM Jun 17 2024
Martin Baturina - Croatia
Picha: Mtandao
Martin Baturina - Croatia

Ni miaka 20 tangu Wayne Rooney kutoka England alipotangaza kipaji chake kwa ulimwengu kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya 2004.

Nani mwingine atakuwa nyota chipukizi katika michuano ya Ulaya msimu huu wa majira ya kati ya wachezaji wote 622?

Hapa BBC Sport inawachambua wachezaji wachanga wa kutazamwa msimu huu wa majira ya joto Ujerumani.

Martin Baturina - Croatia

Baturina ameicheze Croatia mechi tatu hadi sasa.

Ana umri wa miaka 21. Mchezaji kiungo wa klabu ya Dinamo Zagreb na raia wa Croatia. Ni maarufu nchini kwake na amepewa jina la 'The Next Modric'!

Timu yake ni washindi wa ligi ya Crotia, na hataweza kudumu muda mrefu zaidi baada ya Euro, kwani Juventus na Arsenal zinamtaka na sio wao pekee.

Warren Zaire-Emery - Ufaransa

Ana umri wa miaka18, anacheza kiungo katika klabu ya PSG.

Amefanya vizuri akiwa na klabu hiyo msimu huu na kupata tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka na mkataba mpya hadi 2029.

Benjamin Sesko - Slovenia

Ana umri wa miaka 21, ni mshambuliaji wa klabu RB Leipzig ya Ujerumani.

Sesko ni mshambuliaji mwenye mwenye futi 6 na inchi 5 ambaye mashabiki wa Arsenal wanamfahamu kwa sababu ambapo anahusishwa kutaka kujiunga nao kwa pauni milioni 50 kutoka RB Leipzig.

Aliondoka Red Bull Salzburg kwa mkopo hadi Leipzig. Aliifungia Salzburg mabao 18 msimu wa 2022-23.

Brian Brobbey – Uholanzi

Brobbey amepewa jina la utani 'Brobbeast' tangu siku zake za awali akiwa Ajax.

Ana umri wa miaka 22 ni mshambuliaji wa klabu ya Ajax ya Uholanzi.

Brobbey ameifunga Ajax mabao 22 katika mashindano yote. Katika kampeni ambayo wababe hao wa Uholanzi walikuwa chini kabisa ya kwenye msimamo, mchango wake uliwafikisha kufika nafasi ya tano.

Na tayari ameonja mafanikio katika ngazi ya kimataifa, akishinda mara kwa mara mashindano ya Ulaya ya Vijana chini ya miaka 17 mwaka 2018 na 2019.

Florian Wirtz - Ujerumani

Ana umri wa miaka 21, anachezea katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Ni moja wa vijana wawili wa umri wa miaka 21 katika timu ya Ujerumani ambao wanajulikana sana na mashabiki wa Uingereza kutokana na ushujaa wao katika klabu.

Wirtz amekuwa mbunifu katika timu ya Leverkusen iliyotwaa ubingwa chini ya Xabi Alonso, ingawa alikosa kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar kutokana na jeraha la goti.

Ameanza mechi saba kati ya nane tangu Julian Nagelsmann achukue usukani mwaka jana, haswa akiwa upande wa kushoto wa washambuliaji watatu.

Giorgi Mamadashvili - Georgia

Umri wake ni miaka 23, ni kipa wa klabu ya Valencia ya nchini Hispania, anachukuliwa na wengi kuwa kipa bora kijana katika soka la Ulaya.

Mamardashvili amekuwa chaguo la kwanza kwa nchi yake, na kacheza mechi 13 za mwisho za kimashindano ya kimataifa.

Johan Bakayoko - Ubelgiji

Ana umri wa miaka 21, ni mshambuliaji wa kulia wa timu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. Alihamia PSV Eindhoven akiwa na umri wa miaka 16 kutoka Anderlecht na amefanya vyema akiwa na PSV kwa kushinda taji akiwa na mabao 16 na pasi za mwisho 14.

Majira ya joto yaliyopita ilisemekana alitakiwa na Brentford na Burnley, mwaka huu ni Bayern, Arsenal na Liverpool - inaweza kuwa vigumu kwa PSV kukataa ofa kutoka klabu hizo.

Georgiy Sudakov - Ukraine

Umri wake ni miaka 21, ni mchezaji kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

Shakhtar Donetsk ilikataa ombi la kumuuza kwa Napoli Januari, lakini Sudakov anasema ni wakati wa kuiondoa familia yake kwenye vita na huenda akaenda London kwani amekuwa akihusishwa na klabu za Arsenal, Tottenham Hotspur na Chelsea.

Jamal Musiala - Ujerumani

Musiala amepewa jina la utani 'Bambi' kwa sababu ya uwezo wake wa ajabu wa kupiga chenga.

Ana umri wa miaka 21, nafasi yake ni kiungo katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

Ndiye nyota mwingine mchanga wa Ujerumani. Inashangaza kwamba Musiala, ambaye alikulia London na kuiwakilisha Englandal kwenye timu ya taifa chini ya umri wa miaka 21, tayari yuko kwenye michuano ya tatu kwa Ujerumani.

Alianza kucheza Euro 2020 akiwa na umri wa miaka 18.

Joao Neves - Ureno

Umri wake ni miaka 19. Kiungo wa klabu ya Benfica. Hakukosa hata dakika moja ya msimu uliopita akiwa Benfica, alicheza kila sekunde katika michezo 12 ya Ulaya.

Alipata nafasi baada ya Enzo Fernandez alipoondoka Lisbon na kwenda Chelsea 2023. Benfica wanataka zaidi ya pauni milioni 80 kumuuza.

Ikiwa atafanya vizuri kwenye Euro 2024, kunaweza kuwa na foleni ya klabu kubisha hodi kwenye mlango wa wakala Jorge Mendes.

Strahinja Pavlovic - Serbia

Umri wake ni miaka 23. Ni beki wa kati wa klabu ya Red Bull Salzburg. Pavlovic amekaa kwa misimu miwili Red Bull Salzburg baada ya kusajiliwa kutoka Monaco.

Ana uwezekano wa kuanza upande wa kushoto wa safu ya kati ya wachezaji watatu wa Serbia.

Leopold Querfeld - Austria

Querfeld amekuwa akihusishwa kujiunga Crystal Palace, Rangers ama Celtic.

Ana umri wa miaka 20. Ni beki wa kati wa Rapid Vienna. Kwa jina la utani 'Ukuta wa Austria.'

Querfeld amekuwa beki mzuri kwa Rapid Vienna katika misimu miwili iliyopita, na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa.

Arda Guler - Uturuki

Umri wake ni miaka 19. Anacheza kama kiungo katika klabu ya Real Madrid.

Alijiunga na Real kutoka Fenerbahce msimu uliopita wa majira ya joto lakini akajeruhiwa vibaya, na hakucheza mchezo wowote mpaka mwishoni mwa Januari.

Akiwa na mabao sita katika mechi 12 za kwanza alizochezea akiwa na Madrid. Kocha wa Uturuki, Vincenzo Montella lazima ashawishike kumwanzisha kwenye michuano ya Ulaya.

Xavi Simons - Uholanzi

Umri wake ni miaka 21. Ni mshambuliaji wa PSG. Alifanya vyema akiwa kwa mkopo katika klabu ya RB Leipzig kutoka PSG msimu huu.

Alikuwa mchezaji aliyechezewa vibaya zaidi katika Bundesliga msimu huu, anapenda kuwa mtoa huduma kwa wachezaji wenzake, akimaliza nafasi ya pili kwa pasi za mwisho katika Ligi Kuu ya Ujerumani.

Zeno Debast - Ubelgiji

Debast amekuwa katika timu ya Anderlecht tangu 2010

Umri wake ni miaka 20. Ni beki wa Anderlecht/Sporting. Amekuwa Anderlecht tangu 2010, akijiunga na akademi hiyo akiwa na umri wa miaka sita, lakini alitangaza wiki hii: "Nimeamua kuichezea Sporting Club de Portugal msimu ujao."

Debast alikwenda kwenye Kombe la Dunia 2022 na kupata uzoefu wa mashindano, ingawa hakucheza sana.

Mario Mitaj - Albania

Umri wake ni miaka 20. Ni beki wa kushoto wa Lokomotiv Moscow. Baada ya mafanikio yake katika klabu ya AEK Athens, na misimu miwili yenye mafanikio sana akiwa na Lokomotiv Moscow ilifuata. Juventus wanaripotiwa kumtaka.

Vladyslav Vanat - Ukraine

Umri wake ni miaka 22. Ni mshambuliaji wa Dynamo Kiev. Akiwa amebarikiwa na kasi na udhibiti, Vanat alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Ujerumani Juni mwaka jana.

Alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kusalia Kiev.

Jeremie Frimpong – Uholanzi

Frimpong alijiunga na Manchester City akiwa na umri wa miaka tisa na kukaa na klabu hiyo kwa miaka tisa kabla ya kujiunga na Celtic mwaka wa 2019. Alihamia Leverkusen mwaka 2021

Umri wake ni miaka 23. Mshambuliaji wa kulia au beki wa kulia wa Bayer Leverkusen. Amefunga mabao 14 na kutajwa katika timu bora ya Bundesliga kwa mwaka wa pili mfululizo.

Alitumiwa kama winga ya kulia na Ronald Koeman na kupata matokeo mazuri katika mechi ya kirafiki ya Uholanzi dhidi ya Canada, ambapo alifunga bao na kusaidia.

Alikuwa sehemu ya kikosi kwenye Kombe la Dunia la 2022, lakini hakushiriki.

Matej Jurasek - Jamhuri ya Czech

Umri wake ni miaka 20. Ni winga wa Slavia Prague. Kwa muda wa angalau miaka amekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora zaidi kutoka Jamhuri ya Czech na bado anaweza kujumuishwa kwenye orodha hii.

Ni mchezaji mzuri kila upande, anaweza kutatizika kupata nafasi ya kuanzia kwenye Euro kwa sababu ya mfumo finyu wa Czech.

Morten Hjulmand - Denmark

Umri wake ni miaka 24. Ni kiungo wa Sporting. Amekuwa sehemu ya timu ya Ruben Amorim iliyoshinda taji la ligi ya Ureno msimu huu.

Ana umri wa miaka 25 baadaye mwezi huu lakini huu haukuwa msimu wake wa kwanza akiwa Sporting na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa Septemba, hivyo bado ni mpya kabisa.

Kenan Yildiz - Uturuki

Yildiz aliisaidia Juventus kuishinda Atalanta katika fainali ya Coppa Italia msimu uliopita

Umri wake ni miaka 19. Ni m shambuliaji wa klabu Juventus. Mzaliwa wa Ujerumani alifunga katika Uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin katika mchezo wake wa kwanza wa kimataifa Novemba wakati Uturuki ilipoishinda Ujerumani katika mji wao mkuu.

Aliondoka Bayern Munich majira ya joto wakati mkataba wake ulipoisha na akakataa ofa kutoka Barcelona, akipendelea kujiunga na Juventus.