Arusha kinara tuzo za walimu, Dar yatoka mikono mitupu

By Restuta James , Nipashe
Published at 12:10 PM Jun 26 2024
Tuzo za walimu zinaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na lilishirikisha walimu wa shule za umma kutoka Halmashauri zote nchini.
Picha: Restuta James
Tuzo za walimu zinaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na lilishirikisha walimu wa shule za umma kutoka Halmashauri zote nchini.

WALIMU watatu wanaotokea mkoani Arusha, wameibuka kidedea kwa kutwaa tuzo tatu za kwanza, kwenye shindano la pili la stadi za kufundisha, ambalo mwaka huu liliangalia somo la Kiingereza kwa shule za msingi.

Tuzo hizo zinaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na lilishirikisha walimu wa shule za umma kutoka Halmashauri zote nchini.

Akieleza azma ya tuzo hizo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Anneth Komba, amesema zinalenga kuwapa walimu motisha na kutambua mchango wao.

Amesema zaidi ya walimu 3,700 walishiriki shindano hilo.

Washindi wa kwanza na wa pili wametokea Enaboishu Academy, ambao ni Jenifer Chuwa (wa kwanza) na Sophia Moses (wa pili) pamoja na Mwalimu Mmasi wa  Shule ya Msingi Tuvaila iliyopo Meru.

Mshindi wa kwanza alizawadiwa Sh. Milioni tatu, wa pili Sh. 2,500,000 na wa tatu Sh. Milioni mbili pamoja na vyeti.

Hakuna mwalimu aliyetokea shule za Dar es Salaam katika 10 kwenye tuzo hizo.

Aidha, walimu wa kike wamekuwa vinara kwani ni walimu wawili wa kiume walioingia kwenye 10 za tuzo hizo.