Ndivyo ukweli matumizi mkono wa kushoto unavyochanganya watafiti

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:55 PM Sep 03 2024
Kuanzia mwaka 1976, kila Agosti 13, dunia inaadhimisha siku maalum ya watu wanaotumia mkono wa kushoto. Rais mstaafu wa Marekani, Barrack  Obama ni baadhi ya watu mashuhuri wanaotumia mkono huo.
PICHA: MTANDAO
Kuanzia mwaka 1976, kila Agosti 13, dunia inaadhimisha siku maalum ya watu wanaotumia mkono wa kushoto. Rais mstaafu wa Marekani, Barrack Obama ni baadhi ya watu mashuhuri wanaotumia mkono huo.

INAPOFIKA Agosti 13 ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wanaotumia mkono wa kushoto.

Hata hivyo, haijafahamika ni kwa nini kuna uwezekano mdogo kwa baadhi ya binadamu wanaotumia mkono wa kushoto kutumia wa kulia. 

Utafiti wa kisayansi wa matumizi ya mkono wa kushoto, unaonyesha taarifa nyingi zaidi kuhusu wanadamu, kuanzia jinsi unavyobadilisha namna ya kufikiria.

Aidha, kuna wale ambao wanaweza kutumia "upande wa kushoto," lakini mara hii kwa maana ya kusikia, na sio kwa mkono.

Yupo mtu anatumia mkono wa kushoto tangu utotoni, hasa wakati anapoanza kushikilia kitu na kushika kalamu kuandika kwenye karatasi. 

KUSHOTO NI BORA? 

Ni nini hufanya mkono mmoja kuutawala mwingine, na kwa nini watu wanaotumia mkono wa kushoto ni wachache?

Maelezo yanayohusiana na mada hii ni zaidi ya watu walivyofikiria. Kwa mfano, hatukutambua hapo awali kwamba utegemezi wa mtu kwa mkono mmoja zaidi kuliko mwingine ni jambo ambalo pia linaenea kwenye viungo vingine. Mfano macho.

Kila mmoja anaweza kutambua kama yeye ni mtumiaji wa mkono wa kushoto kupitia majaribio yafuatayo:

Kuna mfano wa kujaribu: Nyoosha mkono mmoja na ushikilie kidole gumba mbele yako. Kisha angalia kwa macho yote mawili na kisha kwa kila jicho wakati ukifunika jicho lingine. 

Jicho lako lenye nguvu litakuwa lile linalokuruhusu kuona kidole karibu na muundo wake wa asili zaidi.

Unaweza pia kujaribu masikio yako ili kuona ni lipi unalotumia mara moja na kwa urahisi zaidi wakati wa kuongea na simu.

Ni jambo la kushangaza kuona haya yanatokea katika maisha halisi. Mara nyingi, wapo wanaoshikilia simu mkono wa kushoto na kuiweka kwa shida sikio la  kulia, wakati unaandika haraka  kwa na mkono wa kulia

Kwa ujumla, asilimia 40 ya binadamu husikia vizuri kwa sikio la kushoto, asilimia 30 wanaona vizuri kwa jicho la kushoto na asilimia 20 wana mguu wa kushoto wenye nguvu kuliko wa kulia.

Jambo la kushangaza ni kwamba asilimia ya chini sana linapokuja suala la wale ambao "wanatumia mkono wa kushoto", kwani asilimia yao haizidi 10 ya idadi ya watu.  

KWA NINI?

Inasemekana hapo zamani waliokuwa wanatumia mkono huo walifokewa na kufukuzwa kwa sauti kubwa na kuonekana kuwa wanatia aibu.

Mfano wakiwa wanafunzi shuleni au kwenye shughuli za kijamii walichukuliwa kama watu walio kinyume na njia ya asili.

Hata leo hata hakuna maelezo mabaya yanayohusishwa na mkono wa kushoto ambayo bado yanaendelea katika lugha nyingine.

Neno la Kiingereza "kushoto" linatokana na lugha ya Waanglo-Saxon ambalo liliandikwa  lyft na lilimaanisha "dhaifu." 

Neno kinyume cha "kushoto" katika Kilatini ni ‘dexter, maana yake "mkono wa kulia" na lilihusishwa na ustadi, uadilifu, ucha mungu, na haki.

Kwa hivyo ni nini kinachoamua kuwa mtu atakuwa anatumia zaidi mkono wa kushoto? Kwa mtazamo wa mabadiliko, ni rahisi zaidi kufahamu sababu za kutumia mkono mmoja kuliko mwingine. 

Kwa upande wa nyani wana uwezo wa kugawa kazi fulani kwa mkono mmoja.

Sokwe huchagua "mkono" ambao anaona unafaa zaidi kati ya viungo vyake na kuuingiza kwenye shimo ambapo wadudu wanaishi, kwani hisia ya kugusa humpa habari nyingi juu ya kina na upana wa shimo na jinsi lilivyo na mchwa ambao wana ladha kwa aina hii ya tumbili.

Kisha sokwe huvuta "mkono" wake kwa urahisi, akifunua mawindo yake, ambapo hujaribu kulazimisha kuingiza taya shimoni.

Kwa kutumia mkono huo huo kufanya kazi hiyo, kila wakati hula mchwa wengi.

Lakini, utafiti uliofanywa na wanasayansi wa nyani na sokwe wa porini umeonyesha kuwa matumizi yao ya viungo ni tofauti na binadamu.

Katika kila kazi ambayo watafiti waliifanya kuwahusu sokwe, ilionyesha kuwa nusu ya sokwe walitumia "mkono wa kulia" kuifanya, wakati nusu nyingine walitumia wa kushoto, yaani, uwiano wa asilimia 50 kwa 50, ambayo inaleta swali.

Katika hatua gani kwenye mageuzi yetu wale wanaotumia mkono wa kulia kimsingi walionekana kuwa wengi zaidi kuliko wenzao wa mkono wa kushoto? Mtu mmoja kati ya 10 anatumia mkono wa kushoto?

Meno ya binadamu wa kale ‘Neanderthals’ ni kiashiria muhimu katika suala hili. Inaonekana kuwa mtu huyu alikuwa na akili na mwenye busara kwa wakati mmoja.

Mababu hao walitumia meno yao kushikilia vipande vya nyama ili kuzikata kwa kisu kilichoshikiliwa mkono wa kulia.

Alama hii ya kushoto kwenye meno ya mbele na kwa kuchunguza alama hizi, wanasayansi waliamua ni mkono gani ulioshikilia kisu na ambao ulishikilia nyama.

La kushangaza, uchunguzi huo ulifunua kuwa uwiano wa mkono wa kushoto na wa kulia kati ya wanadamu hawa wa zamani ulikuwa sawa na uwiano kati yao leo, mmoja hadi 10.

Hata hivyo, inajulikana kwamba kuna msingi wa maumbile. Hata hivyo, wanasayansi katika uwanja huu bado wanajaribu kutambua sehemu maalum za nasaba (DNA) zinazohusika na hili, na idadi ya jeni zinazoaminika kuwa na jukumu katika suala hili kufikia jeni 40 tofauti.

Kwa kuzingatia data ya sasa, hatuwezi kujua sababu maalum kwa nini watu wengine wanatumia mkono mmoja zaidi kuliko mwingine, wala hatuna maelezo ya ni kwa nini "watu wa wanaotumia mkono wa kushoto" ni wachache. Kwa hivyo, jibu la swali lolote katika suala hili linabaki kuwa "halijapatikana."

Lakini je, kutumia mkono wa kushoto kuna athari yoyote kwa maisha ya mtu, isipokuwa ugumu? Sivyo, katika kushika mkasi ambao umeundwa kwa matumizi na mkono wa kushoto au zipu ambayo mtu hawezi kuifunga, au kalamu ambayo inashikika vizuri kwa mkono wa kulia? Hakuna jibu.