WACHEZAJI wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani wamebainika huku Ligi Kuu England (EPL), ikiendelea kutawala.
Kampuni ya Utafiti wa Michezo ya Deloitte Football Money imechapisha data kuhusu klabu 30 tajiri zaidi duniani ambazo zinajivunia mapato makubwa zaidi katika msimu wa 2023/24, na rekodi mpya iliyowekwa ya euro bilioni moja.
Hapa tunaziangalia klabu 30 tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa Deloitte, twende sasa...
NAFASI YA 30-21
Klabu za Ligi Kuu England zinaunda timu nyingi kati ya kumi zinazoongoza, lakini pia hushiriki kwa urahisi ndani ya 30 bora.
Wolverhampton Wanderers, Fulham, Everton na Crystal Palace zimejumuishwa kutoka 29 hadi 26 kwa mpangilio huo, kwa mara nyingine tena kuangazia misuli ya kifedha ya Waingereza.
Brighton & Hove Albion imeendelea kupaa juu (sasa ni ya 21) kutokana na mtindo wao wa kuvutia wa biashara ambao unalenga kununua wachezaji wa bei ya chini na kuuza kwa bei juu. Ushiriki wa 'Seagulls' hao kwenye Ligi ya Europa 2023/24 pia umeongeza mapato.
Flamengo ndio timu pekee nje ya Ulaya iliyojumuishwa katika 30 bora, iliingia kwenye orodha ikiwa na mapato ya chini ya euro milioni 200. Miamba hao wa Brazil watatarajia kucheza Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia msimu huu wa kiangazi jambo ambalo litawapa fedha zaidi.
Benfica ndio timu pekee ya Ulaya nje ya Ligi Kuu tano kushiriki na ipo katika nafasi ya 25. Mapato yao yaliboreshwa mbele ya AS Roma na Napoli za Italia, pamoja na Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.
30. Flamengo euro milioni 198.2
29. Wolves euro milioni 206.9
28. Fulham euro milioni 212.2
27. Everton euro milioni 217.6
26. Crystal Palace euro milioni 218.9
25. Benfica euro milioni 224.0
24. Eintracht Frankfurt euro milioni 245.2
23. Roma euro milioni 249.0
22.Napoli euro milioni 253.6
21. Brighton euro milioni 256.8
NAFASI 20-11
Klabu nyingine tatu za Ligi Kuu England ziko nje ya kumi bora, huku Aston Villa na West Ham United zikishika nafasi ya 18 na 17. Zote zilipata zaidi ya euro milioni 300 msimu wa 2023/24.
Newcastle United ilipata manufaa kwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2023/24, na kupata euro milioni 371.8 katika kipindi chote cha kampeni. Hilo ni ongezeko la kuvutia la asilimia 29 kutoka msimu uliopita na watakuwa na nia ya kuongeza mapato zaidi ya kifedha kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Soka la Ufaransa haliko katika hali nzuri zaidi ya kiafya, lakini mabeberu wa jadi, Lyon na Marseille zote zimo katika 20 bora. Timu hizo zilifurahia msimu wa 2023/24 wenye matokeo mazuri, huku mapato yao yakiongezeka kwa asilimia 33 kutoka msimu wa 2022/23.
Inashangaza kwamba hakuna timu za Italia zilizojumuishwa katika kumi bora, huku AC Milan, Inter na Juventus zikiwa chini ya jedwali. Miamba wa Turin ni miongoni mwa timu chache ambazo zilipoteza fedha msimu uliopita – euro milioni 78.2 kuwa sahihi - na zimeporomoka hadi nafasi ya 16, huku klabu zote mbili za Milan zikifurahia ongezeko la wastani la asilimia tatu ya mapato.
Atletico Madrid iliyopo nafasi ya 12 pia ilifurahia ongezeko la mapato kwa msimu wa 2023/24, lakini mapato yao bado ni madogo ikilinganishwa na wapinzani wao wa LaLiga. Mbio za fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zilikuwa bora kwa ongezeko la fedha kwa Borussia Dortmund, ambao walipata mapato ya zaidi ya euro nusu bilioni.
20. Lyon euro milioni 264.1
19. Marseille euro milioni 287.0
18. Aston Villa euro milioni 310.2
17. West Ham United euro milioni 322.2
16. Juventus euro milioni 355.7
15. Newcastle United euro milioni 371.8
14. Inter euro milioni 391.0
13. AC Milan euro milioni 397.6
12. Atletico Madrid euro milioni 409.5
11. Borussia Dortmund euro milioni 513.7
NAFASI YA 10-1
Klabu sita za Ligi Kuu England 'wakubwa sita' zote zimeingia kwenye kumi bora na timu ya Chelsea iliyokuwa na matumizi makubwa zaidi imepata fedha kidogo zaidi. Ilipata euro milioni 545.5 katika mapato msimu uliopita, chini ya wapinzani wao wa London Tottenham Hitspur ambao walitengeneza euro milioni 615.
Liverpool imeporomoka hadi nafasi ya nane katika viwango vya ubora, ikiachwa na Arsenal ambayo imeruka kutoka nafasi ya kumi hadi ya saba. Majukumu hayo yanaweza kubatilishwa hadi mwisho wa kampeni ya sasa, lakini ongezeko la mapato la asilimia 35 kwa 'Washikabunduki' hao litafurahisha uongozi wa klabu hiyo.
Barcelona na Bayern Munich ziko karibu sana katika nafasi ya sita na ya tano, na hali mbaya ya kiuchumi kwa 'Wakatalunya' hao imewafanya kupoteza euro milioni 39.8 kuliko ilivyokuwa 2022/23. Bayern huwa wanapata mapato thabiti na wamepanda katika viwango licha ya masuala yao ya uwanjani msimu uliopita.
Manchester United inaweza kuwa katika hali mbaya uwanjani, lakini imepanda kwenye orodha kutokana na ongezeko lao la mapato la euro milioni 24.9. Hata hivyo, bado inacheza na wapinzani wao, Manchester City, ambao walipata euro milioni 67.2 zaidi ya 'Mashetani Wekundu' msimu uliopita wakiwa njiani kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Paris Saint-Germain kwa sasa ipo katika nafasi ya tatu kutokana na kuondoshwa kwa nyota wao wakuu katika miaka ya hivi karibuni, lakini hakuna anayekaribia kuinasa Real Madrid.
Mabingwa hao watetezi wa Ulaya waliimarishwa na ukarabati wa Santiago Bernabeu ambao uliwaruhusu kupata mapato ya euro bilioni moja kwa msimu mmoja ambayo ni rekodi mpya.
10. Chelsea euro milioni 545.5
9. Tottenham euro milioni 615.0
8. Liverpool euro milioni 714.7
7. Arsenal euro milioni 716.5
6. Barcelona euro milioni 760.3
5. Bayern Munich euro milioni 765.4
4. Manchester United euro milioni 770.6
3. Paris Saint-Germain euro milioni 805.9
2. Manchester City euro milioni 837.8
1. Real Madrid euro bilioni 1.05
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED