RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, anaanza ziara ya siku sita nchini Korea. Ni tukio linalotazamwa ndani yake kinabeba sura pana ya uhusiano kisasa, kihistoria, undugu, pia diplomasia uchumi ambayo ndio sera na muongozo mkuu wa Tanzania nje ya mipaka.
Suala la uwekezaji katika sekta ya kilimo kuwa mlishaji taifa na hata nguzo ya kuajiri, Korea Kusini ina undugu wa kitaifa, tangu mikakati ya awali ya uchumi wa nchi, katika Serikali ya Awamu ya Kwanza.
Ziara ya sasa ya Dk. Samia, anatarajiwa kurejea nchini na mambo makuu matatu; mikataba saba ya maendeleo, pia mkataba wa mkopo nafuu Dola za Marekani Bn. 2.5 sawa na Sh.Trilioni 6.5 za kuwekeza katika miudombinu, elimu na afya kama alivyodokeza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa,
Pia, anatarajiwa kurejea na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Anga Korea (KAU). Hadi sasa
ana zingime kama hizo alizopewa na vyuo vikuu vya Dar es Salaam (UDSM), Zanzibar (SUZA) nchini, pia Jawaharal Nehru (India), Ankara (Uturuki).
Ni jambo lionalomuanika Rais Dk. Samia, mbali na uzoefu kikazi, kitaaluma, kichwani alivyowekeza darasa la elimu ya takwimu katika ngazi ya diploma nchini, pia stashahada ya uzamili katika uchumi, huko Manchester Uingereza, leo anayotenda yanayomuonyesha stadi yake katika fani uchumi, ameiva.
Hiyo ni mara baada ya kukakalia nafasi ya urais, Dk. Samia hakuficha dhana yake kusimamia mambo makuu matatu katika mikakati ya uchumi wa Tanzania nje ya mipaka.
Rais ambaye wiki hii anazawadiwa stashahada ya udaktari wa falsafa ya tano, kutoka Chuo Kikuu cha Anga (KAU) nchini Korea Kusini, anapigania kuimarisha Tanzania ing’are katika diplomasia uchumi, ziara zake zimekuwa zikilenga kunasa masoko ya bidhaa za nyumbani ughaibuni.
Vyuo vikuu vilivyompa tuzo kama hiyo ya uzamivu vya Dar es Salaam (UDSM), Zanzibar (SUZA) nchini, pia Jawaharal Nehru (India), Ankara (Uturuki).
Maeneo mengine alikojipanga kukuza uchumi kimkakati nchini, ni pakukaribisha uwekezaji mitaji hasa ya viwanda na kwenye kilimo na ushirikiano wa jumuiya/urafiki kimataifa, wakati huohuo, ikinakshi nchi kwa urafiki kisiasa.
Neema zinashuhudiwa, pale misaada ya kifedha, uwekezaji na jina la nchi kimataifa kilipaa, mahsusi hata mwenyewe Rais, imekuwa kama sheria ndogo, kila anakoalikwa au kufanya ziara ni kawaida anakaribishwa kuwasilisha ama mada, hotuba au kuongoza kikao. Si haba, Tanzania inang’ara kupitia Mama ‘anayeupiga mwingi.’
TANZANIA ILIKOTOKA NAO
Tangu zama za uongozi wa Awamu ya Kwanza uongozi wa Tanzania na Korea Kusini, zimekuwa na historia kusaidiana kuwapo miradi hasa ya kilimo, ikijumuisha kusomeshwa Watanzania elimu ngazi hadi ya shahada za juu.
Pia, nchi hiyo imekuwa na baadhi ya miradi ya kilimo katika mikoa kama ya Morogoro, tena ikitumia wataalamu wengi wasomi Watanzania wahitimu wa nchi hiyo.
Ni aina ya uhusiano endelevu kufika zama za sasa, katika Awamu ya Nne ya uongozi wa nchi, taifa hilo la ukanda wa Mashariki ya Dunia, ikitia saini yamiradi ya kilimo nchini.
SAMIA VS KOREA KUSINI
Mkakati wa Rais Dk. Samia, katika falsafa yake ya kujenga Tanzania yenye kilimo cha kisasa na biashara, Julai mwaka jana zimeingia katika makubaliano ya kushirikiana kufanyika utafiti wa kilimo chenye teknolojia ya kisasa, ambayo katika miaka miwili ya mfululizo bungeni, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amekuwa akiinadi.
Nchi za Tanzania na Korea Kusini, hadi sasa zimeshakubaliana kushirikiana katika kuimarisha utafiti wa kilimo na matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kilimo, ili kuongeza tija kwa wakulima nchini, mwaaka huu.
Hapo kukafafanuliwa lengo la kuwapo tija kwa wakulima shambani, jijini Jeonju-si, Korea Kusini, katika mazungumzo ya Naibu Waziri wa Kilimo wa Tanzania Anthony Mavunde na Yun Jongchul, Makamu Mtawala Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo na Utafiti ya Korea (Korea Patnership for Innovation in Agriculture - KOPIA).
Kupitia mazungumzo hayo, Naibu Waziri Mavunde akaiomba KOPIA kuanzisha kituo chake nchini Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), ili kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi katika utafiti kilimo, lengo ni kumsaidia mkulima kufikia tija ya uzalishaji shambani.
Hapo kunazugumziwa maeneo ya mbegu bora na teknolojia ya kisasa ya kilimo, huku kukiombwa ushirikano wa kitaalamu katika utekelezaji wa Programu ya Vijana – BBT (Building a Better Tomorrow).
Yun Jongchul, Makamu Mtawala Mkuu wa KOPIA anampongeza Rais Dk. Samia Suluhu, kwa utashi wake kukuza kilimo kwa kuiongezea bajeti, naye akiahidi wao KOPIA, wako tayari kushirikiana na kuanzisha kituo chao nchini, kukuza utafiti kilimo na matumizi ya teknolojia kisasa, hasa kwa BBT.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Togolani Mavura, akaishukuru taasisi ya KOPIA kwa utayari wake kufanya kazi na Tanzania, akiahidi kusimamia makubaliano hayo ya kuanzishw kituo hicho, ikiwa ni sehemu ya kutekekeleza ajenda ya kilimo Tanzania.
Ni katika mwendelezo wa ishara kama hiyo, Waziri Mkuu akakutana na ujumbe kutoka Korea Kusini, Septemba mwaka jana, kujadili mikakati ya ushirikiano wa maendeleo kwa pamoja.
Ni sura ya ushirikoano inayorejea tena Januri mwaka huu, pale Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, akisema jijini Dodoma kwamba, ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini umechochea kwa kiasi kikubwa utekelezaj wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, ikiwamo mradi wa kimkakati wa daraja la Tanzanite, Dar es Salaam, lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Korea Kusini, kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF).
Ilikuwa kauli yake waziri, wakati wa kutia saini makubaliano yaliyohusisha Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi ya National Agency for Adminstrative City Construction and Heerim Architects and Planners ya nchini Korea Kusini, ikisanifu na ujenzi nchini wa majengo na miundombinu, jijini Dodoma.
Hapo akarejea uhusiano huo unadhihirishwa pia na ziara za viongozi wa ngazi ya juu (wakati huo) katika mataifa hayo mawili; moja ilifanywa Oktoba 2022, kwa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa.
"Akiwa Korea Kusini Mheshimiwa Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) aliitembelea National Agency for Administrative City Construction. Taasisi hii ni wakala wa kitaifa nchini Korea Kusini inayosimamia na kuendeleza ujenzi wa jiji la Sejong nchini humo.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa taasisi hii Nchini Tanzania ili kubadilishana uzoefu na viongozi wa taasisi zinazofanana na hizi hapa kwetu Tanzania,” akasema Waziri Jenista
Miezi minne baadaye, nako kukashuhudiwa Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) na wanachama wake, wakishuhudiwa wanashiriki Mkutano wa Kibiashara nchini Korea Kusini.
Kwa maana hiyo, ziara ya Rais Dk. Samia, ambayo inaendana na kuingia mikataba zaidi ya saba,vilevile zinailetea nchi fedha za maendeleo Sh.trilion 6.5.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED