10 - bora ya usajili wa majira ya joto hadi sasa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:02 AM Jul 29 2024
Kylian Mbappe kwenda Real Madrid.
Picha:Mtandao
Kylian Mbappe kwenda Real Madrid.

INGAWA Euro 2024 na Copa America zimetawala vichwa vya habari vya soka kwa sehemu kubwa ya majira ya joto hadi sasa, bado kumekuwa na uhamisho mwingi ambao umeweza kuwafanya mashabiki wa soka kufurahishwa pia.

Kuanzia Manchester United hatimaye kuonesha umahiri sokoni, hadi Real Madrid kumsajili mwanasoka bora wa dunia, mashabiki wameona uhamisho mwingi wa kufurahisha ukifanywa.

Hawa ndio wachezaji wetu 10 bora waliosajiliwa msimu huu wa kiangazi hadi sasa... 

10. Daichi Kamada kwenda Crystal Palace (Ada: Huru)

Crystal Palace walinufaika katika hali ya kutoelewana kati ya Daichi Kamada na Lazio msimu huu wa majira ya joto, na kumnyakua mchezaji huyo wa Kimataifa wa Japan bila malipo baada ya mazungumzo kuvunjika na timu hiyo ya Serie A.

Ingawa si kipaji cha kuvutia machoni kama Michael Olise anayeondoka, Kamada hakika ni nyongeza nzuri kwa safu ya ushambuliaji ya Palace, na mchezaji huyo hapo awali alicheza soka bora zaidi maishani mwake chini ya Oliver Glasner kule Eintracht Frankfurt. 

9. Archie Gray kwenda Tottenham Hotspur (Ada: Pauni Mil. 30)

Kwa kocha yeyote mahiri anafahamu kikamilifu kwamba Archie Gray ni mmoja wapo wa vijana wanaotarajiwa kusisimua katika mchezo huo.

Akiwa amekamilisha msimu mzima wa kwanza wenye mafanikio katika soka la kulipwa akiwa na klabu ya utotoni ya Leeds United mnamo 2023/24, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, alijipatia fedha nyingi kwenda kwa wababe wa Ligi Kuu England, Tottenham Hotspur msimu huu.

Uwezo wake wa kucheza beki wa kulia na kiungo wa kati utakuwa muhimu sana kwa kocha Ange Postecoglou. 

8. Alvaro Morata kwenda AC Milan (Ada: Pauni Milioni 10.9)

Pauni milioni 10.9 kwa mshambuliaji ambaye ni nahodha wa taifa lake hadi kutwaa ubingwa wa Euro 2024 na kufunga mabao 21 katika michuano yote msimu wa 2023/24? Ndio, hiyo ni biashara.

Juu ya kiwango kizuri cha Morata kwa Atletico Madrid na Hispania, fowadi huyo pia analeta uzoefu wake Serie A kutoka kwa klabu ya zamani ya Juventus hadi AC Milan, na uwezo wa kuziba pengo la Olivier Giroud katika kitengo cha ushambuliaji cha timu hiyo. 

7. Savio kwenda Manchester City (Ada: Pauni Milioni 30.8)

Kiufundi, Manchester City walilipa klabu ya Troyes pauni milioni 30.8 kwa Savio.

Kwa kweli, kwa sababu ya muundo wa timu ni kama walijilipa pauni milioni 30.8 kwa Savio.

Bila kujali hali mbaya ya kifedha ya uhamisho huu, Man City walionekana kusajili mchezaji mmoja. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa anaitumikia Girona, klabu nyingine ya CFG, katika msimu mzima wa 2023/24, akiwaongoza kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yao na mchango wake wa mabao 19 kwenye La Liga. 

6. Joshua Zirkzee kwenda Man United (Ada: Pauni Mil. 35)

Mshambuliaji anayelinganishwa na Zlatan Ibrahimovic kutokana na ubora wake katika kumiliki mpira, ni sawa na kusema kwamba mashabiki wa Man United wamefurahishwa na usajili wa Joshua Zirkzee.

Zirkzee alikuwa wa kipekee kwa Bologna msimu uliopita, na kwa kuzingatia umri na wasifu wake, 'Mashetani Wekundu' hao wametumia pauni milioni 35 kupata huduma yake inaonekana kama biashara ya bei nafuu. 

5. Leny Yoro kwenda Manchester United (Ada: Pauni Milioni 52.2)

Pauni milioni 52.2, si ada ya kumlipa kijana wa miaka 18, lakini Leny Yoro anaweza kuwa maalum.

Pamoja na kuwa na uwezo sawa wa kumiliki mpira, Man United wamepata huduma ya mchezaji ambaye anaweza kuongoza safu ya ulinzi ya timu hiyo kwa miaka 15 ijayo.

Unapozingatia hilo, labda si bei mbaya baada ya yote. 

4. Joao Palhinha kwenda Bayern Munich (Ada: Pauni Milioni 47.1)

Baada ya kukaribia kusajiliwa katika siku ya mwisho ya majira ya joto - alisafiri kwa ndege kwenda Munich kwa uchunguzi wake kabla ya kujua kuwa mpango haukuweza kukamilika - Joao Palhinha sasa, rasmi ni mchezaji wa Bayern Munich.

Nyota huyo wa Ureno, ambaye alicheza mara nyingi zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Ligi Kuu England kwa miaka miwili iliyopita, ndiye kiungo bora katika safu ya kiungo ya Bayern Munich. 

3. Douglas Luiz kwenda Juventus (Ada: Pauni Milioni 42.4)

Kumuondoa Adrien Rabiot ilikuwa biashara kubwa yenyewe na Juventus, lakini badala yake na kumchukua Douglas Luiz? Kweli, hiyo ni biashara nzuri ya kushangaza.

Mbrazil huyo alikuwa mmoja wa kiungo bora zaidi katika Ligi Kuu England msimu wa 2023/24, na atakuwa mchezaji ambaye Thiago Motta atajenga safu yake mpya ya kiungo ya Juve. 

2. Michael Olise kwenda Bayern Munich (Ada: Pauni Milioni 50.8)

Kimsingi kila klabu kubwa barani Ulaya ilitaka kumsajili Michael Olise. Na ukizingatia ukweli kwamba ana umri wa miaka 22 tu, na alifunga mabao 16 katika mechi 14 tu alizoanza msimu uliopita akiwa na Crystal Palace.

Kwa Olise, Bayern wamesajili mchezaji ambaye ana uwezo wa kuwa wa kiwango cha kimataifa, na mchezaji ambaye anaweza kuleta alama nyingi. 

1. Kylian Mbappe kwenda Real Madrid

Bila shaka uhamisho wa Kylian Mbappe kwenda Real Madrid ndio mkubwa zaidi ya orodha hii. Real Madrid walimsajili mwanasoka bora zaidi duniani kwa uhamisho huru.