Wasimamizi uchaguzi serikali za mitaa waonywa

By Elizabeth Seleman , Nipashe
Published at 05:16 PM Oct 04 2024
Sanduku la kura.
Picha:Mtandao
Sanduku la kura.

HALMASHAURI ya Sengerema mkoani Mwanza, imewataka wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa waadilifu na kujiepusha na udanganyifu kipindi chote cha uchaguzi.

Onyo hilo limetolea leo Oktoba 4,2024 na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri ya Sengerema, Binuru Shekidele, wakati wa kuwaapisha kiapo cha utii wasimamizi hao vilivyotolewa na Kamishana wa Viapo, Christopher Mbuba.

Amewataka kuheshimu viapo hivyo kwani zoezi la uchanguzi ni muhimu na ni vyema wakafuata miongozo kama walivyopatiwa katika mafunzo ya awali.

Shekidele amesema hakuna msimamizi msaidizi atakayevumiliwa kwa kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi huo na kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

 Aidha, amewataka kutoa elimu kwa wananchi kuelekea kwenye uchanguzi huo wa Serikali za Mitaa na kuwaeleza juu ya uboreshaji wa Daftari la Wakazi ulimalizika kwa sasa hatua za kuomba kugombea nafasi mbalimbali kwenye maeneo yao kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya TAMISEMI.

 Aidha amesema iwapo wasimamizi hao watafikisha elimu sahihi kwa wapiga kura hakuta kuwa na upotoshaji, lakini pia wananchi wengi watajitokeza kujiandikisha ili kupiga kura kwenye uchanguzi.