Warioba: Nchi imetulia 4R za Samia zinafanya kazi

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 03:25 PM Oct 04 2024
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba
Picha:Mtandao
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema bado anayaona mafanikio ya falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya R nne (4R) anazozitumia katika utawala wake na kuifanyia nchi kuwa katika utulivu.

Aidha amesema falsafa ya maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reforms), Ustahimilivu (Resilience) na Kujenga upya (Rebuilding), inaendelea kufanya kazi licha ya kuwapo changamoto chache hasa kisiasa. 

Warioba amesema hayo leo Oktoba 4,2024, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa nchi imetulia kisiasa tofauti na miaka mitatu iliyopita. 

Amesema changamoto za kisiasa ni kama kuna mapambano kwa serikai na wapinzania ambao hawawasilishi hoja ipasavyo, huku akishauri wanasiasa kukaa meza moja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Amani inajengwa na wananchi wenyewe na sio polisi, kwasababu hata tulipopata uhuru hatukutumia mtutu wa bunduki bali kwa amani.Polisi wanaposikia maandamano yametangazwa alafu wanasema wanalinda amani wajifakari kwa kuwa ulinzi wa nchi unatokana na wananchi wenyewe bila kujali taasisi moja,”amesema.