Tanzania yashiriki Mkutano wa Maendeleo endelevu wa Hamburg Ujerumani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:45 PM Oct 07 2024
Tanzania yashiriki Mkutano wa Maendeleo endelevu wa Hamburg Ujerumani
Picha: Mpigapicha Wetu
Tanzania yashiriki Mkutano wa Maendeleo endelevu wa Hamburg Ujerumani

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (Hamburg Sustainability Conference) unaofanyika Hamburg Ujerumani ambao umefunguliwa rasmi na Chancellor wa Ujerumani Olaf Scholz leo Oktoba 07, 2024.

Kwenye mkutano huo, Aweso ameandamana na Hassani Iddi Mwamweta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Mkutano huo umewakutanisha Marais, Mawaziri Wakuu, Rais wa Benki ya Dunia, Wakuu wa Taasisi za Kifedha kama IMF, Mawaziri, watu mashuhuri na Taasisi mbalimbali za maswala ya Maendeleo duniani.

Pamoja na mambo mengine Mkutano huu unalenga kuwaleta pamoja wadau wote kutoka Sekta za Umma na binafsi kwa ajili ya kuunganisha nguvu ikiwemo upatikanaji wa Fedha ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endevu (SDGs).