WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamaganda Kabudi, amesema serikali imeamua kuutambua rasmi muziki wa singeli kama alama ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kabudi amesema baada ya kufuatilia kwa kina wameona muziki huo utaitambulisha nchi vizuri.
"Wizara na nchi imeamua tuchukue muziki mmoja na kuufanya alama ya Tanzania, hii haina maana kuwa muziki mwingine imewekwa kando.
“Ila tumeona imefika wakati tujitanabaishe kama taifa ili dunia ikisikia wimbo huo inajua ni Tanzania," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED