Mwenyekiti BAZECHA aomba radhi kauli za udini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:15 PM Oct 04 2024
MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) Hashim Juma.

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) Hashim Juma, ameomba radhi kauli za udini alizozitoa katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Oktoba mosi, 2024.

“Wakati natoa hotuba hiyo ambayo ilikuwa ndefu inakaribia saa 1:30 kwa bahati mbaya kuna sehemu ndogo ambayo ilisambaa kuna baadhi ya watu hawakunielewa walitafisri wanavyoona wao, ilikwanza baadhi ya watu.

“Nami nikaiona clip (picha mjongeo) nikaona hoja za watu mtandaoni kila mtu na uelewa wake na ufahamu wake nichukue nafasi hii na fursa hii kuomba radhi waliokwazika na masuala ya udini, nawaomba radhi sikukusudia hivyo wala kumkwaza mtu yeyote.

Mara baada ya kiongozi huyo kuongea, CHADEMA kupitia Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema walizikana kauli hizo kwamba si msimamo wa chama na wanafuatilia kwa karibu kisha watachukua hatua.

Amesema CHADEMA haihusiki na kauli za kibaguzi za udini, ukabila na ukanda zilizotolewa na kiongozi huyo.